Liverpool yabanwa 0-0 na Birmingham

Liverpool watamshukuru mlinga mlango wao Pepe Reina kwa kuokoa mipira kadhaa iliyokuwa inaingia wavuni katika mechi dhidi ya Birmingham City.

Image caption Pepe Reina aliiwezesha timu yake ya Liverpool kuepuka kipigo kwa kulazimisha sare dhidi ya Birmingham City.

Reina aliokoa mipira kadha ya kichwa ikiwa ni pamoja na ile iliyopigwa na Cameron Jerome na Craig Gardner wakati Liverpool walipozongwa.

Kwa upande wa Liverpool, Fernando Torres aligonga mpira uliookolewa na mlinda mlango Ben Foster katika nafasi adimu waliyopata wakicheza ugenini.

Liverpool walionekana kupata nguvu zaidi wakati Raul Meireles alipoingia kama mchezaji wa akiba, ingawa Liverpool watafurahia pointi hiyo moja waliyopata.

Hata hivyo maswali bado yataendelea kujitokeza kuhusu timu hiyo ambayo mashabiki wake walipata matumaini baada ya Roy Hodgson kuanza kuifunza msimu huu.

Wataalam wa soka wanasema anahitaji muda kuijenga upya baada ya kuirithi kutoka kwa Rafa Benitez aliyehamia Italia.