Msimamo wa Medali Michezo ya Madola

Pamoja na kuonyesha matokeo ya medali za dhahabu/fedha/shaba na jumla ya medali, msimamo huu unaonyesha pia njia mbadala za kutafsiri orodha ya nchi. Ukibofya tabo mojawapo, itabadilisha mwonekano na kuchambua matokeo kwa mujibu wa maelezo hapo chini.

 • Kwenye tabo ya Jumla, msimamo unaonyesha idadi ya medali za shaba, fedha na dhahabu ambazo nchi husika imeshinda katika Michezo ya Jumuiya ya Madola 2010. Safu ya 2006 inaonyesha jumla ya medali ambazo nchi ilishinda kwenye mashindano ya 2006 huko Melbourne, nchini Australia.
 • Kwenye tabo ya Wanaume, namba zinaonyesha idadi ya medali za shaba, fedha na dhahabu ambazo kila nchi imeshinda. Safu ya mwisho inawakilisha asilimia ya jumla ya medali walizoshinda wanaume.
 • Kwenye tabo ya Wanawake, namba zinaonyesha idadi ya medali za shaba, fedha na dhahabu ambazo kila nchi imeshinda. Safu ya mwisho inawakilisha asilimia ya jumla ya medali walizoshinda wanawake.
 • Kwenye tabo ya Washiriki, safu ya 'Idadi ya washiriki kwa medali' inaonyesha jumla ya idadi ya wanamichezo kwa kila nchi ukigawanya na idadi ya medali walizoshinda.
 • Kwenye tabo ya Idadi ya watu, 'Safu ya idadi ya watu kwa medali' inaonyesha jumla ya idadi ya watu kwa nchi ukigawanua kwa jumla ya medali walizoshinda *.
 • Kwenye tabo ya GDP, safu ya 'Pato la nchi kwa medali' inaonyesha Pato la nchi husika ukigawanya kwa jumla ya idadi ya medali walizoshinda*.
 • Kuona idadi ya washiriki kwa kila nchi, idadi ya watu na pato la nchi, bofya safu yake na chagua kisanduku cha mwisho upande wa kulia.

  ‘Pato la nchi kwa medali’ na ‘Idadi ya watu kwa medali’ ni uwiano wa vidokezo tu, na haiwakilishi au kutoa akisi ya kiwango/kiasi cha uwekezaji katika michezo wala watu wanaoshiriki kwenye michezo katika nchi zilizoorodheshwa.

  *Maelezo haya ya kiuchumi yamepatikana kutoka Benki ya Dunia, CIA Factbook na Ofisi ya Takwimu ya Taifa Uingereza.