Liverpool wajikakamua na pointi

Image caption Ryan Babel

Kilabu ya Liverpool ilionekana kuyaacha matatizo yao nyumbani na kuhakikisha wananyakua pointi dhidi ya Napoli katika mashindano ya Europa.

Liverpool walionyesha makali lakini walipoteza nafasi kadha za kufunga mabao kupitia washambulizi kama vile Ryan Babel na David Ngog.

Hata hivyo nusura wangefungwa na Marek Hamsik wa Napoli lakini kwaju lake lilizuliwa na Paul Konchesky kabla ya kuvuka mstari wa goli.

Bila shaka meneja Roy Hodgson atavuta pumzi kwa kuwa timu yake ilikuwa na wachezaji wengi chipukizi na ambao hawana uzoefu mkubwa katika mechi za kiwango hiki.