DIDIER DROGBA

didier
Image caption Didier Drogba

Katika siku ya kwanza la msimu wa ligi ya Uingereza mwaka wa 2009/2010, jambo ambalo kamwe halingetarajiwa lilikuwa linatendeka, mabingwa Chelsea walikuwa waneelekea kushindwa na klabu ya Hull City, lakini ni mabao mawili kutoka kwa Didier Drogba yalionyakulia timu hiyo ushindi.

Bofya hapa kupiga kura:

Na hiyo ndio iliokuwa ishara ya kuwa, mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 32 kutoka Ivory Coast bado alikuwa na mengi ya kuonyesha.

Image caption Didier Drogba

Tangu Januari mwaka wa 2010, Drogba amekuwa akimiminia mabao kwa klabu na nchi yake. Amefungia Chelsea mabao 37 katika mechi 40 na kuiwezesha timu hiyo kushinda ligi ya Uingereza mara mbili mfululizo akiwa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye ligi hiyo.

Kama nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast katika michuano ya Klabu Bingwa barani Africa na Kombe la dunia mwaka wa 2010, Drogba alikuwa mchezaji aliyetoa matumaini zaidi licha ya kuwa timu yake ilishindwa kutamba kwenye mechi zake.

Kinyume na mawazo ya wengi, Drogba amenukuliwa akisema kuwa yeye hana tamaa ya kufunga mabao. Tangu msimu huu uanze amekuwa akiwasaidia wenzake akiwemo Salomon Kalou, Florent Malouda na Mshambuliaji mwenzake Nicholas Anelka kutikisa wavu wa wapinzani wao na mabao.

Drogba ni mmoja wa washambuliaji hatari kwenye ulingo wa kambumbu sasa hivi. Hisia zake kali kuhusu mpira wakati mwengine humsababisha kuwatolea wenzake hasira lakini licha ya hilo, hakuna tashwishi kuwa Drogba ndiye anayetamba uwanjani wakati wowote.

Image caption Didier Drogba

Didier Drogba ndiye anafaa zaidi

Image caption Didier Drogba

Kura yangu ipo kwa Drogba kwa kuwa mchezo wake umekuwa thabiti, na amekuwa akifunga mabao ambayo ni muhimu kwa klabu na taifa lake.

Kama mshambuliaji amedhihirisha kuwa hajakuwa akifunga mabao tuu bali pia amekuwa akiwaandalia wachezaji wenzake nafasi nyingi tuu za kufunga. Hebu waulize Salomon Kalou, Florent Malouda na Nicholas Anelka kwa nini imekuwa rahisi kufunga mabao wakati wanapocheza kwenye upande mmoja naye.

Hakuna mchezaji wa mpira barani Afrika amekuwa na mwaka mzuri kama mshambuliaji huyu kutoka Ivory Coast. Aliuanza kwa mikiki na amemaliza akiwa bado yupo juu.

Mabao yake 37 katika mechi 40 yaliwezesha timu yake ya Chelsea kushinda ligi ya Uingereza mara mbili mfululizo naye akawa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi kwenye ligi hiyo.

Image caption Didier Drogba

Timu ya taifa ya Ivory Coast haikufanya vyema nchini Angola kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika, lakini umahiri wa Drogba ulijitokeza katika mechi za timu yake hadi pale walipong'olewa katika roba fainali za michuano hiyo.

Awali kulikuwa na hofu ikiwa atashiriki kwenye mechi za Kombe la Dunia pale alipovunjika mkono mwezi Juni tarehe 5, lakini ukakamavu wake ulijitokeza kwenye mechi zote za kundi lao huko Afrika kusini.

Ivory Coast walikuwa kwenye kundi lenye timu zenye uzoefu mkubwa, lakini bila shaka Drogba aliaacha sifa kwa bao lake alilofunga kwa ustadi kutumia kichwa ingawa timu yake ilifungwa mabao tatu kwa moja na Brazil.

Mpende au umchukie, kunatofauti kubwa kati ya mshambuliaji na anayefunga mabao, lakini bila shaka utapendezwa zaidi kuwa na anayefunga mabao kwenye timu yako kuliko anayesifika tuu kwa kuandaa mabao.

Ni kipofu tuu atakaye mnyima Didier Drogba, nafasi ya kushinda tuzo hili la mchezaji bora wa soka wa BBC kwa mwaka wa pili mfululizo.