YAYA TOURE

Yaya
Image caption Yaya Toure

Kufuatia kutunukiwa tuzo nyingi mwaka 2009, huo ndio mwaka ambao Yaya Toure aliweza kuthibitisha kwamba yeye ni kati ya wachezaji hodari zaidi duniani.

Bofya hapa kupiga kura:

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, na ambaye uwanjani hucheza kama mlinzi, aliruhusiwa kuondoka Uhispania ambako alikuwa akiichezea Barcelona, na kuingia katika ligi kuu ya England, alipojiunga na Manchester City, akipata mshahara wa kushangaza; pauni 221,000 kwa wiki.

Alijiongezea sifa zaidi wakati alipoifungia nchi yake ya Ivory Coast bao katika michuano ya Kombe la Dunia.

Image caption Yaya Toure

Toure aliondoka Barcelona mara tu baada ya klabu kujipatia ushindi wake wa pili katika La Liga, ingawa nafasi yake ya ulinzi ilimwendea mchezaji Sergio Busquets.

Lakini alipata nafasi ya kuimarika tena, aliposajiliwa na Man City kwa malipo ya pauni milioni 24, akitia saini mkataba wa miaka mitano, na wenye thamani ya pauni milioni 55.

Meneja wa City, Roberto Mancini, alisema kusainiwa kwa Toure ni usajili wa ‘ajabu’.

Image caption Yaya Toure

Mara moja alipata nafasi ya kustawi katika klabu, katika kuimarika hadi kufikia nafasi ya nne bora katika orodha ya ligi ya Premier.

Ingawa Ivory Coast ingelipenda kuyasahau mashindano yaliyopita ya Ivory Coast, Toure alifanikiwa kucheza katika kila dakika ya mechi tatu ambazo nchi yake ilicheza.

Mbali na kuiwezesha timu yake ya Elephants (Tembo) kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Korea ya Kaskazini, alisaidia pia kumfikishia mpira Didier Drogba, aliyeweza kupata bao la kujiliwaza, wakati walipofungwa magoli 3-1 na Brazil.