Blackburn yaishinda Villa 2-0

Morten Gamst Pedersen aliweza kuifungia timu yake ya Blackburn magoli mawili, katika uwanja wa nyumbani Ewood Park, ilipocheza na Aston Villa siku ya Jumapili.

Image caption Morten Gamst Pedersen alijitahidi kuiangusha Villa 2-0

Wamiliki wapya wa klabu ya Blackburn,Venkateshwara na Balaji Rao walikuwa uwanjani kutizama klabu yao mpya ikipata ushindi.

Pedersen alipata bao lake la kwanza kupitia mkwaju ambao ilitazamiwa kipa Brad Friedel alikuwa na uwezo wa kuuzuia, na baadaye aliweza kuuelekeza mpira wavuni, baada ya kuupokea kutoka kwa Ryan Nelsen.

Kipa wa Blackburn Paul Robinson pia alifanya juhudi kuzia mkwaju kutoka kwa Steward Downing, na vile vile Ashley Young aliyejaribu kufunga kwa kichwa.

Mchezaji Robert Pires leo pia alipata nafasi ya kuichezea Aston Villa kwa mara ya kwanza, baada ya kuingia kama mchezaji wa zamu, katika kipindi cha pili.

Lakini kufikia wakati huo, Villa tayari walikuwa wanaongoza kwa magoli 2-0, na kumaliza majivuno ya Villa ya kucheza mechi tano mfululizo pasipo kushindwa.

Meneja Sam Allardyce alianza mechi akiiongoza Blackburn Rovers ikiwa imo katika nafasi ya 16, lakini kufuatia ushindi wa leo, Rover imeruka hadi kufika nafasi ya 11.