Real Madrid yashinda Copa Del Rey kwa kuichapa Barcelona kwa bao 1-0. Bao hilo pekee limefungwa na Cristiano Ronaldo

Real Madrid imeichapa Barcelona bao 1-0 na kunyakua kombe la kwanza katika msimu wa soka nchini Uhispania.

Bao pekee la Christiano Ronaldo katika dakika za nyongeza ndio limeipa Real ushindi huo.

Real Madrid na Barcelona zitakutana tena mara mbili katika mchuano wa kuwania kucheza nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.