Hiddink huenda akaondoka Uturuki

Chama cha soka nchini Uturuki, kimethibitisha Guus Hiddink ana mipango ya kuondoka kama kocha wa timu ya taifa, na huenda akarudi tena katika klabu ya Chelsea kama meneja.

Kulingana na afisa mmoja wa cheo cha juu katika shirikisho hilo, TFF, Hiddink, raia wa Uholanzi, amesema "hatuwezi kuiambia Chelsea la, kwa kuwa tunaamini anataka kuondoka".

Haki miliki ya picha 1
Image caption Huenda akarudi Chelsea

Hiddink, mwenye umri wa miaka 64, aliongoza Chelsea hadi kupata ushindi wa Kombe la FA, alipokuwa meneja wa muda mwaka 2009.

Licha ya kampeni ngumu ya kufuzu kwa michuano ya Euro mwaka 2012, Uturuki bado ina matumaini ya kufuzu kwa mashindano hayo, baada ya sare ya 1-1 siku ya Jumamosi dhidi ya Ubelgiji.

Despite an indifferent qualifying campaign, Turkey remain in contention for a Euro 2012 play-off place after a 1-1 draw against Belgium on Saturday.

Lakini Hiddink hana raha tena kutokana na kwamba mtu aliyemfanya kuikubali kazi hiyo mjini Istanbul, Mahmut Ozgener, mkuu wa shirikisho hilo, huenda akaondolewa katika uchaguzi wa rais wa kuliongoza shirikisho, tarehe 28 mwezi Juni.

"Ikiwa Ozgener atabaki, kuna uwezekano Guus pia angelibaki", alielezea afisa huyo.