Murray amshinda Mfaransa Tsonga

Andy Murray ameibuka bingwa katika mashindano ya tennis ya Aegon Championship, na ikiwa ni njia bora ya kuyakaribisha mashindano ya kuchezea katika viwanja vya nyasi msimu huu, kwa kumshinda Jo-Wilfred Tsonga katika uwanja wa Queens, mjini London.

Haki miliki ya picha B
Image caption Bingwa wa mwaka 2011 mashindano ya Aegon Championships

Murray alipata ushindi wa 3-6 7-6 na 6-4.

Pambano hilo lilicheleweshwa kwa siku moja, baada ya mvua kuzuia mambo siku ya Jumapili.

Murray amesema ushindi huo hautapunguza ugumu wa kupata ushindi katika mashindano ya Wimbledon yanayokuja, na atafanya kazi ya ziada kujiandaa kwa mashindano hayo.

Ameelezea kwamba ikiwa atakuwa katika hali nzuri, ana uwezo wa kupata ushindi wa Wimbledon.

Waandalizi wa mashindano hayo waliweza kuuza tiketi zaidi kwa wenyeji na wapenzi wa tennis usiku wa Jumapili, na nyingine siku ya Jumatatu, kufuatia mvua kusitisha fainali hiyo hapo mwanzo.

Murray aliwahi kupata ubingwa wa mashindano hayo mwaka 2009.

.