Korea ya kusini kuandaa Olimpiki

Mji wa PyeongChang ulishinda katika duru ya kwanza ya kikao cha Kamati ya IOC mjini Durban, ikiushinda mji wa Munich wa Ujerumani pamoja na mji wa pwani ya Ufaransa wa Annecy.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwenyeji wa Olimpiki majira ya baridi

Hii ni mara ya tatu kwa Korea ya kusini kushiriki pata shika ya kuwania nafasi ya kuandaa michezo ya Olimpiki na ni maana kwamba nchi hiyo imefanikiwa kuandaa babu kubwa ya mashindano makubwa duniani.

Itakumbukwa kuwa mashindano ya michezo ya majira ya joto ya Olimpiki yalifanyika nchini humo mnamo mwaka 1988, vilevile Kombe la Dunia la mwaka 2002, kisha yatafuata mashindano ya Dunia ya riadha yatakayofanyika mjini Daegu mwezi ujao, halikadhalika hivi sasa orodha hiyo inaongezewa mashindano ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka 2018.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Olimpiki mwaka 2018

Ushindi huu licha ya kuwa unaelekea Korea ya Kusini kuna mkono wa Muingereza hapa kupitia meneja uhusiano Mike Lee, ambaye hapo kabla alishughulikia mradi wa London kuwa mwenyeji wa mashindano ya Oilimpiki ya mwaka ujao wa 2012, Rio de Janeiro mwaka 2016 na mpango wa Qatar wa kuandaa fainaliza Kombe la Dunia mwaka 2022.