Imebadilishwa: 6 Julai, 2011 - Saa 03:55 GMT

Blatter:Afrika imarisheni mchezo wenu

Bwana Blatter na Rais Zuma.

Rais wa Fifa Sepp Blatter amesema kuwa nchi za Afrika lazima ziimarishe mchezo wake kama wanataka nafasi za bara hili kuongezwa katika michuano ya Kombe la Dunia.

Nchi sita ziliwakilisha bara la Afrika katika Kombe la Dunia mwaka uliopita kwa kuwa Afrika Kusini walikuwa wenyeji.

Hakuna tena timu ndogo,kila mmoja anaweza kumfunga mwenzake, lakini ni jukumu la bara Afrika kuonyesha kuwa linastahili kupata nafasi zaidi.

Sepp Blatter

Lakini nafasi za bara hili zitarudi kuwa tano katika fainali za mwaka 2014 nchini Brazil.

Kumekuwa na wito kutoka kwa baadhi ya nchi za Afrika wakitaka nafasi za uwakilishi ziongezwe.

Lakini Rais wa Fifa anasema Afrika lazima iimarishe mchezo wake ili kupata fursa ya nafasi zaidi.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana

" Kila mjumbe wa Fifa ana haki sawa katika kupiga kura,lakini inapofika Kombe la Dunia,ikiwa ni uwekezaji mkubwa wa Fifa,kamati yetu kuu imekubaliana kuwa yale mashirika ya soka yenye viwago vya juu vya mchezo ndiyo yawe na waakilishi wengi zaidi," Blatter alisema akiwa mjini Harare.

" Mustakabali wenu unategemea matokeo ya timu za Afrika katika Kombe la Dunia."

Matokeo ya Afrika mwaka 2010, ambapo ni Ghana pekee ilifika kwenye hatua ya robo fainali,ni hatua ya juu zaidi kwa nchi ya Afrika kuwahi kufika katika Kombe la Dunia.

Cameroon na Senegal pia zimewahi kufika katika hatua ya robo fainali mwaka 1990 na 2002 mtawalia.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.