Liverpool kumsajili Charlie Adam

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchezaji Charlie Adam

Liverpool imekubaliana na Blackpool kuhusu kuhama kwa mchezaji Charlie Adam.

Adam, mwenye umri wa miaka 25, amewasili kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na kujadiliana kuhusu masuala yake binafsi.

Mwezi Januari alikuwa karibu ajiunge na Tottenham lakini muda wa kuhama kwa wachezaji ukamalizika kabla ya wao kuafikiana kuhusu kandarasi yoyote.

Iwapo Adam atajiunga na Liverpool, atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na meneja Kenny Dalglish tangu walipomaliza katika nafasi ya sita kwenye ligi kuu ya England msimu uliopita.

Mchezaji mwengine, Jordan Henderson, alijiunga na Liverpool kutoka Sunderland mwezi Juni kwa kiasi cha pauni za Uingereza milioni £20m.

Golikipa wa Roma Alexander Doni pia huenda akajiunga na Liverpool katika saa 36 zijazo, haya ni kwa mujibu wa wakala wake Ovidio Colucci.

Timu zote zilikubaliana kuhusu kuhama kwa Doni mwezi uliopita lakini walikuwa hawajakubaliana kuhusu masharti yake binafsi.