Chelsea yalalamikia Malaysia kwa ubaguzi.

Yossi Benayoun
Image caption Yossi Benayoun

Chelsea yalalamikia Malaysia kwa ubaguzi dhidi ya Benayoun.

Chelsea imelalamika kwa chama cha mpira cha Malaysian kuhusu jinsi mchezaji wao Yossi Benayoun alivyokabiliwa na matamshi ya kibaguzi wakati wa mechi ya kirafiki mnamo wiki iliyopita.

Beayoun ambae ni Muisraeli alizomewa kila mara alipogusa mpira katika mechi kati ya Chelsea na timu ya Malaysia Julai 21 .

Chelsea imesema : "tunaamini Yossi alilengwa na mashabiki kadhaa na matamshi ya ubaguzi dhidi ya Wayahudi.

"tabia hiyo inachukiza na haikubaliki kamwe katika sokal," ikaongeza taarifa ya Chelsea.

Mashirika ya habari yakiiripoti kuhusu mechi hiyo iliyochezwa Kuala Lumpur yalisema Benayoun alilengwa na matamshi ya kibaguzi- akiwa miongoni mwa Waisraeli wachache kucheza nchini Malaysia, nchi ambayo haiitambui Israeli.