Mkenya Patrick Makau avunja rekodi

Patrick Makau ahifadhi ubingwa wake katika mbio za Marathon za Berlin kwa kuvunja rekodi ya dunia.

Haki miliki ya picha internet
Image caption Patrick Makau akitimka Berlin

Mwanariadha huyo wa Kenya alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa mbili ,dakika tatu na sekunde 38. Makau alikuwa amevunja rekodi hiyo ya Muethiopia Haile Gebreselassie kwa sekunde 12.

Bingwa huyo wa Ethiopia alishindwa kumaliza mbio hizo kutokana na matatizo ya tumbo yalionza kumsumbua baada ya kukimbia kwa 27 km..

"wakati wa asubuhi mwili wangu haukuwa katika hali nzuri , lakini baada ya kuanza kukimbia , mwili wangu ukaanza kuwa mzuri . Nikaanza kuwaza juu ya rekodi ya dunia", Makau alisema.

Gebresalassie, mwenye umri wa miaka 38 ambaye ni bingwa mara mbili wa mbio za 10,000m alikuwa amepanga kundikisha muda bora utakomuwezesha kufaulu kushiriki katika mashindano ya Olimpki ya mjini London.

Haki miliki ya picha internet
Image caption Gebresellasie akiwa na maumivu

Lakini Muethiopia huyo alilazimika kuyaaga mashindano hayo pale alipofika nusu ya mbio hizo.

Wakala wake Jos Herman alidokeza kuwa Gebresallasie alikuwa na matatizo ya pumu. Ingawa alikuwa ameruhusiwa kutumia madawa ,lakini mwamba huyo amekuwa hatumii madawa kwa muda mrefu kwani amekuwa hana matatizo yeyote ya kiafya

Sasa Gebrselassie anapanga kusafiri hadi Dubai kwa mbio nyengine za marathon ili kuhakikisha kuwa ameandikisha muda wa kasi utakaomuwezesha kushiriki katika mashindano ya Olimpik ya mjini London.