El Amrani Katibu Mkuu mpya Caf

El Amrani
Image caption Hicham El Amrani

Hicham El Amrani amethibitishwa kuwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka barani Afrika Caf.

Uamuzi huo umechukuliwa na kamati kuu ya Caf kwenye mkutano uliofanyika mjini Cairo, Misri.

El Amrani mwenye umri wa miaka 32, alijiunga na shirikiho hilo mwezi Machi 2009 kama naibu katibu mkuu.

Amrani amekuwa akikaimu nafasi hiyo tangu mwezi Oktoba mwaka jana, baada ya kuondoka kwa Mustapha Fahmy aliyekwenda Fifa kuwa mkurugenzi wa mashindano.

Alikuwa mkuu wa idara ya masoko katika shirikisho la soka la bara Asia kabla ya kujiunga na Caf.