Tottenham hotspurs yaepuka aibu.

Katika michuano ya Ligi ya Europa zilizochezwa alhamisi usiku, timu ya Tottenham Hotspurs ya uingereza iliponea kuadhibiwa na Shamrock Rover ya Ireland kabla ya kujikusanya na kufunga magoli matatu ya haraka haraka.

Ingawa Hotspurs ilishinda mechi hiyo kwa mabao 3 - 1 lakini Shamrock ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga.

Katika dakika ya 50 Stephen Rice aliifungia Shamrock goli.

Bao hilo liliwafanya Tothenham kushambulia lango la Klabu ya Shamrock na kufaulu kufunga mabao matatu katika muda wa dakika tano tu.

Waliofunga walikuwa Roman Pavlyuchenko katika dakika ya 60, dakika moja baadae Jermain Defoe akafanya mabao kuwa mawili na katika dakika ya 60 Giovani dos Santos alikamilisha kibarua kwa kufunga bao la tatu.

Naye Mchezaji wa kimataifa wa kenya ,Victor Mugabe Wanyama , ambaye ni nduguye mdogo MacDonal Mariga wa Real Sociedad ya Uhispania alipokea kadi ya njano katika hali ya kuisaidia klabu chake cha Celtic ya Ireland kutofungwa na Udinese ya Italy.

Celtic waliokuwa wakiongoza kwa 1-0 waliwakasirisha mashabiki wao wapatao 37,000 pale bao hilo lilipokombolewa kwa njia ya penalti kukiwa kumesalia dakika saba mechi kumalizika.

Sare hiyo imeiwacha Celtic ikivuta mkia katika kundi I.

Katika michuano hiyo ya Ligi ya Europa ,Stoke City ya Uingereza iliizoa alama tatu katika mechi za kundi E baada ya kuifunga timu ya Besiktas ya Uturuki.

Mabao ya Stoke yalifungwa na Peter Crouch na Jon Walters.

Timu nyegine ya uingereza Fulhama ilipata ushindi wa 2-0 kwa kuwa aibisha wenyeji wao Odense BK ya Denmark .

Mabao yote ya Fulham yalifungwa na Andy Johnson.

Kwengineko timu ya Sporting Lisbon ya Ureno wakiwa wamesalia na wachezaji 10 waliweza kuwafungua Lazio ya Italy 2-1.

Kwa ushindi huo wa Sporting Lisbon inaongoza kundi D kwa alama sita baada ya kucheza mechi mbili.

Mabao yaliofungwa na Igor Gabilondo na Markel Susaeta iliipatia Athletic Bilbao ushindi wa 2-0 win dhidi ya Paris St Germain.

Ilikuwa ni siku ya mkosi kwa Paris St Germain kwani mchezaji wao Mohamed Sissoko alitolewa baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 53 ya mechi hiyo.