Corinthians kutomfuatilia Tevez tena

Tevez Haki miliki ya picha AP
Image caption Carlos Tevez

Meneja mkuu wa Klabu ya Corinthians Edu ameiambia BBC klabu yake haina mipango ya kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez.

Tevez alikuwa akisakwa na klabu hiyo ya Brazil iliyokuwa tayari kutoa pauni milioni 35, lakini hawakuweza kufanikisha mkataba huo kutokana na kuishiwa muda.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa sasa amesimamishwa kucheza wakati timu yake ikifanya uchunguzi wa tuhuma kuwa alikataa kucheza dhidi ya Bayern Munich.

"Kwa sasa hakuna mipango ya kujaribu kumsajili tena," amesmea Edu ambaye aliwahi pia kuichezea Arsenal na timu ya taifa ya Brazil.

"Naanza kufikiria kikosi chetu cha mwaka 2012 na nimezungumza na kocha wetu kuhusu wachezaji tunaowataka - lakini Tevez Hayumo". Amesema Edu.