Rooney afungiwa mechi tatu

Rooney
Image caption Wayne Rooney

Mshambuliaji wa England Wayne Rooney amefungiwa kucheza mechi tatu za michuano ya Euro 2012 ngazi ya makundi kufuatia kupewa kadi nyekundi katika mchezo dhidi ya Montenegro.

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka la Ulaya, ilifikia uamuzi huo katika kikao kilichofanyika siku ya alhamisi.

Michuano ya Euro 2012 itafanyika mwakani katika nchi za Poland na Ukraine.

Rooney, 25, alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia rafu Miodrag Dzudovic katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2.

Inafahamika kuwa chama cha soka cha England kitakata rufaa.

Katika ligi kuu ya England, adhabu ya kosa kama hilo ni kuzuiwa kucheza mechi tatu.

Lakini sera za Uefa ni kumpiga marufuku mchezaji mechi moja, na baadaye kamati kutazama kila kosa kivyake, na kama ikibidi, kutoa adhabu zaidi.

Badala ya kutoa adhabu ndefu ya kuzuiwa kucheza, Uefa ilikuwa na uwezo wa kutoa onyo au kupiga faini.