Man City bado kileleni

Manchester City, licha ya kushambuliwa vikali na Wolves katika dakika 14 za mwisho wa mchezo, na wakiwa na wachezaji 10 uwanjani, waliweza kutetea vikali nafasi yao katika kuongoza ligi wakiwa juu kwa point tano zaidi, na walipoondoka kwa ushindi wa magoli 3-1.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meneja wa Manchester City bila shaka anawaza msimu huu ana silaha zote kumwezesha kupata ubingwa wa ligi

Man City kufikia sasa inaongoza ligi kuu ya Premier ikiwa na pointi 28.

Edin Dzeko aliiwezesha City kutangulia kwa bao kutokana na kosa la Wayne Hennessey, aliyeshindwa kuzuia mkwaju wa David Silva, na Aleksandar Kolarov akifanikiwa kutia mpira wavuni.

Lakini Vincent Kompany alionyeshwa kadi nyekundu kwa kucheza vibaya, na kufuatia nafasi ya penalti iliyojitokeza, Stephen Hunt aliwapa Wolves matumaini.

Hata hivyo, bao la mpira unaokwenda kwa kupinda hewani kutoka kwa Adam Johnson ulithibitisha wazi Man City wanahitaji magoli, na wakiwa na nia ya kufanya vyema zaidi katika ligi ya mwaka huu.

Katika viwanja vingine vya mechi iliyochezwa sambamba na hii, Norwich ilitoka sare ya magoli 3-3 ilipoikaribisha Blackburn.

Sunderland pia iliridhika kwa sare ya magoli 2-2 ilipopambana na Aston Villa.

Swansea iliifunga Bolton magoli 3-1.

Wigan haikuwa na lake ilipocheza uwanja wa nyumbani, kwani ilifungwa magoli 2-0.

Katika mechi nyingine za awali, Arsenal ikicheza ugenini iliishinda Chelsea magoli 5-3, huku Everton ikishindwa na Manchester United goli 1-0.

Mechi ya mwisho Jumamosi katika ratiba ni mchezo wa West Brom na Liverpool.