Rwanda yateua kocha mpya

Rwanda Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rwanda yapata kocha mpya

Miluntin Sredojevic kutoka Serbia ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Rwanda, na kuchukua nafasi ya Sellas Tetteh kutoka Ghana.

Sredojevic, kocha wa zamani wa Sudan atakuwa na wasaidizi watatu raia wa Rwanda, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka la Rwanda, FERWAFA.

Tetteh alijiuzulu kufuatia shutuma zilizotokana na Rwanda kushindwa kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika 2012.

Rwanda ilishinda mchezo mmoja tu kati ya mitano huku mchezo wa mwisho wakichapwa 5-0 na Ivory Coast wakiwa nyumbani.

Kujiuzulu kwa Tetteh kulifuatiwa na kujiuzulu kwa rais wa FERWAFA, Jenerali Jean Bosco Kazura, ambaye nafasi yake ilizibwa wiki mbili zilizopita na Celestin Ntagugira.