Man City waifunza mpira Villareal.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yaya Toure na mwenzake washerehekea bao

Wakati Man United wakisumbuliwa na na Otelul Galati, mahasimu wao Man City walikuwa wakiwafunza mpira Villareal nyumbani kwaoUhispania.

Yaya Toure aliipatia Manchester City magoli mawili na kuiongezea matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo ya klabu bingwa bara Ulaya.

Ingawa Man City walikuwa wanacheza kama watu walio uwanjani kwao wakifanya mazoezi ,lakini walitoka uwanjani wakiwa na hofu baada ya mchezaji wao matata David Silva kuondoka uwanjani akiwa na maumivu mgongoni.

Olympique Lyon 0-2 Real Madrid

Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili na kuipatia Real Madrid ushindi wa mabao mawili na wenyeji wao Olympique Lyon ya Ufaransa sufuri.

Ajax Amsterdam 4-0 Dynamo Zagreb.

Nayo Ajax Amsterdam iliwachapa wageni wao Dynamo Zagreb 4-0 .

Hivyo Real Madrid wanaongoza kundi D na pointi 12 wakifuatwa na Ajax Amsterdam na alama 7.

Bayern Munich 3-2 Napoli.

Bayern Munich waliwafunga wageni wao Napoli ya Italy 3-2.

Kwa ushindi huo Bayern iko kileleni mwa kundi A na pointi 10 wakifuatwa na Manchester City na pointi 7. Villarreal ni ya mwisho.