Salman Butt akata rufaa miezi 30 jela

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya kriketi ya Pakistan Salman Butt amewasilisha rufaa dhidi ya adhabu ya miezi 30 jela kutokana na kula njama ya kuvuruga mchezo kwa makusudi baada ya kupokea fedha, wakili wake alisema.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Salman Butt mahakamani London tarehe 3 Novemba, 2011

Alitiwa hatiani mwaka jana baada ya mechi dhidi ya England.

Mchezaji mwengine Mohammad Asif, alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na Mohammad Amir, yeye alipewa kifungo cha miezi sita kutona nao kushiriki kwa namna moja au nyingine.

Wakala wa kriketi Mazhar Majeed alifungwa miaka miwili na miezi minane jela.

Wakili Yasin Patel amethibitisha rufaa ya Butt.

Mwezi wa Februari wachezaji hao wote watatu walifungiwa kucheza kriket kwa muda wa miaka mitano na Baraza la Kimataifa la Kriketi. Wote wamekata rufaa kupinga adhabu hiyo ya kufungiwa.

Wachezaji hao walikamatwa baada ya mechi baina ya Pakistan na England mwezi wa Agosti mwaka 2010.