Mchezaji wa Nigeria Elejiko afariki dunia

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Nigeria Bobsam Elejiko, alianguka uwanjani na kufariki dunia wakati akiichezea timu yake ya Ubelgiji ya Merksem SC siku ya Jumapili.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bobsam Elejiko afariki dunia uwanjani

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa akicheza mechi dhidi ya FC Kaart wakati alipoanguka na kupoteza fahamu.

Majaribio ya kuuzindua moyo wake yalishindikana na sababu za kifo chake hazijaelezwa mara moja.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Merksem imesema:"Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo kilichotokea ghafla cha Bobsam Elejiko." Mechi hiyo ilisimamishwa baada ya kifo cha Elejiko.

"Alianguka na kufa hapo hapo uwanjani na rambirambi zetu tunazitoa kwa familia yake na marafiki."

Elejiko alishawahi kuchezea klabu za Westerlo na Antwerp.