Huwezi kusikiliza tena

Mchezaji bora zaidi wa soka Afrika 2011

Juhudi za BBC za kumtafuta mchezaji bora zaidi wa soka mwaka 2011 zimeanza siku ya Ijumaa.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Gervinho kutoka Ivory Coast ni kati ya wachezaji wanaowania tuzo ya BBC

Msikilizaji unaweza kushiriki katika kura ya kumtafuta mchezaji huyo.

Shiriki kwa kutuma ujumbe wa SMS, ama piga kura kupitia mtandao.

Andika 1 kumchagua Dede Ayew, 2 ni Samuel Eto'o, 3 ni Gervinho, 4 ni Seydou Keita na andika nambari 5 kumchagua Yaya Toure.

Ayew huichezea Ghana na klabu ya Ufaransa ya Marseille.

Samuel Eto'o ni mchezaji wa Cameroon na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

Gervinho ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Arsenal ya England.

Seydou Keita huichezea Mali na mabingwa wa Ulaya Barcelona.

Yaya Toure ni mchezaji wa Ivory Coast na klabu ya England ya Manchester City.