Arsenal, Barca zawika

Van Persie Haki miliki ya picha PA
Image caption Magoli 18 katika mechi 18 msimu huu

Arsenal imeingia katika ngazi ya makundi ya ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kuichapa Burrusia Dortmund kwa mabao 2-1.

Robin Van Persie alipachika mabao hayo mawili na kuhakikisha Arsenal inaingia kwa mara nyingine tena katika ngazi ya timu 16.

Arsenal inakuwa timu ya kwanza ya England kusonga mbele na pia kumaliza juu katika kundi lao.

Chelsea nayo ilishindwa kutamba mbele ya Bayer Leverkusen baada ya kuzabwa 2-1.

Ili kusonga mbele Chelsea itahitaji sare au kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Valencia.

Barcelona nayo iliishinda AC Milan kwa 3-2.

Katika michezo mingine BATE Borisov ilichapwa 1-0 Plzen, Marseille kufungwa 1-0 na Olympiakos, Shaktar Donetsk kuzabwa 2-0 na FC Porto, Valencia kuiachia kisago 7-0 Genk huku Zenit St Petersburg ikitoka sare ya 0-0 na Apoel Nicosia.