Man City yachapwa, Man U yabanwa

Balotelli Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bao la Balotelli halikuweza kuisaidia sana City

Manchester City ilishindwa kutamba mbele ya Napoli baada ya kuzabwa 2-1. Napoli ndio walianza kupachika bao la kwanza kupitia Edison Cavani.

Mario Balotelli alisawazisha bao hilo, lakini Cavani alizamisha meli ya City kwa kuandika bao la pili. City sasa watalazimika kusibiri matokeo ya mchezo kati ya Napoli na Villareal ili kufahamu hatma yao ya kuingia raundi ya makundi hata kama watashinda mchezo wao dhidi ya Bayern Munich.

Manchester United nayo ililazimishwa sare ya 2-2 na Benfica kwenye uwanja wa Old Trafford. Man United walijifunga katika dakika ya 4 kupitia beki wake Phil Jones. Dimitar Berbatov alisawazisha bao hilo. Darren Fletcher aliandika bao la pili la United dakika ya 59, lakini kabla hata kabla mashabiki hawajamaliza kushangilia Benfica walisawazisha bao hilo katika dakika ya 60.

Benfica sasa wamefuzu. United wanahitaji pointi moja kuzonga mbele.

Real Madrid nayo iliendeleza wimbi lake la ushindi kwa kuikandika Dinamo zagreb 6-2.

Bayern Munich ikaichapa Villareal 3-1, CSKA Moscow ikicheza nyumbani ilifungwa 2-1 na Lille.

Lyon na Ajax zilitoka sare ya 0-0, Otelul Galati nayo ikafungwa na FC Basel 3-2.

Trabzonspor ikatoka sare ya 1-1 na Inter Milan.