Arsenal yabanwa na Fulham

Vermaelen Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vermaelen alifunga magoli mawili lakini matokeo sare

Arsenal imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 1-1 na Fulham.

Beki wa Arsenal Thomas Vermaelen alijifunga mwenyewe na kuipa Fulham bao la kuongoza katika dakika ya 65.

Hata hivyo beki huyo alifuta makosa yake dakika nane baadaye kwa kusawazisha goli hilo kwa kupachika mpira wa kichwa kutokana na krosi iliyopigwa na Theo Walcott.

Kipa wa Fulham Mark Schwarzer, aliokoa mipira kadhaa na kuisaidia klabu yake kupata pointi hiyo muhimu.

Matokeo haya yameisogeza Arsenal nafasi moja na kwenda nafasi ya sita kutoka nafasi ya saba.