Gary Speed ajitoa roho

Chama cha soka cha Wales, (FAW), kimeielezea BBC kwamba inaelekea meneja wa timu ya taifa ya soka, Gary Wales, amejiua mwenyewe.

Maafisa wa polisi wa Cheshire wamethibitisha kwamba alipatika amekufa saa moja za asubuhi na dakika nane, saa za GMT, akiwa nyumbani Huntington, Chester.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Gary Speed aliwahi kuichezea Wales na kuwa nahodha wa timu ya taifa

Wanasema hakuna utata kuhusiana na kifo hicho, na inaelekea alijitoa roho.

Waziri mmoja wa Wales, Carwyn Jones, amesema hizo ni habari za kuhuzunisha na kusikitisha mno.

"Ulimwengu umempoteza Gary Speed, mtu mashuhuri sana, na ninasikitika sana kwa kuwa ni jana asubuhi tu nilizungumza naye. Kwa nini? Kwa nini? Kwa nini? Nitamkosa sana maishani!", aliandika mchezaji mwenzake wa zamani, Robbie Savage, katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

"Kimawazo tuko pamoja na familia yake wakati huu wa maombolezi."

Chama cha soka cha Wales FAW kilitangaza; "Tunatoa rambirambi zetu kwa familia yake".

"Tunawaomba wote kuhiheshimu familia yake na kuwaachia fursa ya kuomboleza wakati huu wa huzuni mno."

Speed, ambaye alipata tuzo ya MBE mwaka 2010 kutokana na jitihada zake katika soka, amemwacha mjane na watoto wawili.

Gary Speed alikuwa na umri wa miaka 42.