Djibout mboga kwa Zimbabwe yalala 2-0

Michuano ya Mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP imendelea mjini Dar es Salaam nchini Tanzania ambapo timu mwalikwa wa mashindano hayo Zimbabwe imeifunga timu ya Djibout kwa magoli 2 -0 katika mchezo wa kundi A.

Haki miliki ya picha
Image caption Zimbabwe yailaza Djibout mabao 2-0

Nazo Zanzibar na Burundi zimetoka sare bila kufungana katika mchezo wa pili wa kundi B.

Ikiwa ni mechi yake ya kwanza Zimbabwe ilionyesha kandanda safi katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam ambapo katika dakika ya 9 kipindi cha kwanza Ngoma Donald baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mavura Timire aliandika bao zuri kabla ya Amini Qadr kufunga bao la pili kwa mkwaju mkali wa adhabu karibu na lango la Djibout.

Katika mchezo wa pili wa mashindano hayo Zanzibar na Burundi zilitoka sare ya kutokufungana. Kutoka sare hiyo kunaiweka Zanzibar katika mazingira magumu ya kusonga mbele katika mashindano hayo kwani hadi hivi sasa ina pointi moja na goli moja tu hivyo italazimika kushinda mechi inayofuata itakapokutana na Somalia.