Nahodha wa Brazil 1982 afariki

Mchezaji mashuhuri wa soka aliyewahi kuwa nahodha wa Timu ya soka ya Brazil, Socrates amefariki akiwa mwenye umri wa miaka 57. Socrates aliyezaliwa tarehe 19/02/1954 alikuwa nahodha wa Timu ya Brazil kwenye michuano ya Kombe la Dunia mara mbili.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Socrates wa Brazil

Jina lake, Socrates Brasileiro Sampaio de Souza Vierra Oliveira. Ni dhana ya babake kua ukiwapa wanao majina ya watu mashuhuri watafuata nyayo zao. Ni mtoto wake wa nne aliyeponyoka jina Xenofontes, baada ya mamake kupinga vikali na badala ya hilo akaitwa Rai aliyeshiriki Timu ya Brazil iliyoshinda Kombe la Dunia la mwaka 1994.

Wakati Socrates akicheza, wengi walimuona kama mchezaji bora wa wakati huo.

Jina lake la Socrates, lilitokana na babake kusisitiza wanawe watatu wapewe majina ya wana filosofia wa Ugiriki ya kale. Akiwa na jina kama hilo haikushangaza kuona mcheza soka huyu kupata sifa ya mtu anayetumia mda wake akitafakari kitu, kutoa maoni yake juu ya masuala mbalimbali pamoja na soka.

Socrates alikuwa Daktari, mwandishi, mchambuzi, mnywaji na mvutaji sigara. Lakini atakumbukwa zaidi kwa kipaji chake cha kucheza soka, na kwa kuwa nahodha wa Timu ya Brazil iliyocheza vizuri lakini ikashindwa Kombe la Dunia.

Socrates hakujali sana mchezo wa soka hadi alipohitimu kama Daktari kutoka Chuoni akiwa mwenye umri wa miaka 23.

Alishamiri alipokua akichezea klabu ya mjini Sao Paolo, Corinthians,ambako pia alikua kinara wa mageuzi akidai wachezaji wahusishwe katika maamuzi ya klabu.

Alishiriki mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza mwaka 1979. Hadi fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1982 nchini Uhispania, alikua ameishapewa jukumu la nahodha. Mwenye umbo refu, bila maringo, mwenye kipaji cha kusakata gozi na jicho la kutafuta magoli.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Socrates alikiri kupenda sigara na kinywaji

Socrates alipenda sigara na aliwahi kukiri kua anapenda sana kinywaji chake(pombe) Alikataa kubadilika, hakutaka kuacha sigara wala pombe. Hata kipindi hiki akikaribia mwisho wa uhai wake alikataa kupendelewa kurushwa foleni ili afanyiwe apasuaji wa kubadili maini. Alisema alitaka atunzwe kama raia wa kawaida. Lakini ukweli ni kwamba hakuwa mcheza soka wa kawaida!!

Socrates amefariki akiwa na umri wa miaka 57 na kuacha mjane na watoto sit.