Huwezi kusikiliza tena

Urunani kupambana Morocco

Timu ya Urunani ya Burundi, mabingwa wa mchezo wa mpira wa kikapu katika ukanda wa Afrika ya Mashariki wamefika Morocco tayari kwa mashindano ya vilabu bingwa Afrika.

Image caption Kina dada wa Burundi kuiwakilisha Afrika Mashariki na Kati katika mashindano ya Morocco

Urunani pamoja na Cooperative Bank ya Kenya ndio walitarajia kuuwakilisha ukanda huo wa tano kwenye mashindano hayo.

Timu 16 kutoka maeneo mbali mbali ya kanda za basketball ndizo zinataraji kushiriki mashindano hayo yanayoanza Jumatatu ambapo droo ilitazamiwa kufanyika Jumapili.

Mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani Kibuga alielezewa na mkurugenzi wa kiufundi wa chama cha baseketball nchini Burundi Christian Manirakiza kuhusu maandalizi ya timu yao, muda mfupi kabla ya Urunani kuondoka mjini Bujumbura, na akisema muhimu ni kwamba sio tu wanaiwakilisha Burundi, bali kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati.