Hatimae Man City yafungwa

Chelsea 2 - 1 Man City

Image caption Lampard asherehekea baada ya kufunga bao

Penalti ya Frank Lampard ndiyo iliyowapa ushindi Chelsea na hii ilikuwa mechi ya kwanza ambayo viongozi wa ligi Manchester City wamepoteza msimu huu.

Lampard - ambaye kwa mara nyingine hakujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha Andre Villas-Boas - aliingizwa kama mchezaji wa akiba na akafunga dakika saba kabla ya mechi kumalizika baada ya Joleon Lescott kuunawa mpira katika eneo la hatari.

Mario Balotelli aliipatia City goli la mapema lakini Chelsea ikasawazisha kupitia Raul Meireles kabla ya mapumziko.

Vijana wa Roberto Mancini walilazimika kubaki wachezaji 10 katika kipindi cha pili wakati Gael Clichy alipoonyeshwa kadi nyekundu, na hapo ndipo Chelsea wakatumia fursa ya idadi yao uwanjani na kujipatia ushindi wa tatu mfululizo huku Manchester City wakiendelea kuongoza lakini kukiwa na tofauti ya alama mbili kati yao na Manchester United walio katika nafasi ya pili.