Droo ya klabu bingwa Ulaya

Bingwa mtetezi wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya Barcelona ilijishindia bahati ya kuchuana na Bayer Leverkusen katika michuano ya 16 za mwisho.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Barcelona na Bayer Leverkussen

Bahati ya Barcelona kuepuka safari ndefu ya kwenda Urussi majira ya baridi kali kwa mchuano dhidi ya CSKA Moskow, wenzao Real Madrid hawakuweza kuepuka bahati ya kisanduku. Dro ya leo imeiweka Real Madrid kwenye safari ya Moskow kuchuana na CSKA Moskow mwezi Febuari.

Dro hiyo imeiona klabu ya England, Arsenal ikionyeshwa safari ya Italia kupambana na AC Milan huku Chelsea ikipangwa na Napoli pia ya Italia.

Image caption Arsenal

Nyingine zitakazoshiriki zitachuana kama ifuatavyo: Marseille na Inter Milan; FC Basel dhidi ya Bayern Munich; Lyon ichuane na APOEL Nicosia; na Zenit St. Petersburg ipambane na Benfica.

Mechi za mkondo wa kwanza zitafanyika kati ya tarehe 14-15 Febuari na 21-22, huku mkondo wa pili ukifanyika kati ya Machi 6-7 na 13-14.

Kwa sababu vilabu viwili vya Urussi vilimaliza katika nafasi ya pili na hivyo havikusajiliwa, ina maana kwamba vilabu viwili vilivyomaliza katika nafasi nzuri vitapata bahati ya kusafiri kwenda Urussi majira ya baridi.

Bila shaka hali ya hewa itachangia majaliwa ya mechi hizo. Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Real Madrid Emilio Butragueno amesema kua itabidi wawe waangalifu.

Mkurugenzi wa klabu ya Milan Umberto Gandini amekumbusha jinsi klabu yake ilivyoondolewa na Arsenal kwenye hatua kama hii mnamo mwaka 2008.

Gandini aliongezea kua ni marudio ya wakati ule Arsenal ilipotuchapa 2-0 kwenye uwanja wa San Siro, kweli mechi itakua nzuri ukizingatia historia hio. Klabu ya kwanza katika historia ya Cyprus kuwahi kufikia hatua hii ya 16 APOEL, ikionekana kama kibonde cha michuano hii imepangwa kuchuana na Lyon ya Ufaransa.

Benfica pia itasafiri kwenda Urussi kupambana na Zenit St. Petersburg, huku Bayern ikipewa safari fupi kuelekea mpakani kwa mchuano dhidi ya Basel ya Uswizi kilomita chache kutoka mpaka wa nchi hizo mbili. Labda Inter ndiyo itakayokua na safari fupi zaidi kuchuana na Marseille nchini Ufaransa.