Huwezi kusikiliza tena

Karateka wakusanyika

Vijana chipukizi zaidi ya 80 ikiwa ni watoto wa umri kati ya miaka 5 hadi 18 kutoka Burundi, Kenya na Rwanda wanakutana kuanzia Jumapili mjini Bujumbura, katika mashindano ya mchezo wa Karate.

Haki miliki ya picha ii
Image caption Afrika Kaskazini kwa sasa inasemekana ni bora zaidi kwa karate zaidi ya Afrika Mashariki

Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga anaelezea dhamira ya michezo hiyo ni kukagua na kukuza vipaji vya karate katika kanda, kuanzia umri mdogo na kujipima baadaye na nchi za Afrika ya Kaskazini zilizopiga hatua kubwa katika mchezo wa Karate.

Kibuga amezungumza na kocha kutoka Kenya, Elizabeth Muthoni Rukwaro.

Amemuelezea Kibuga kwamba wakati huu ambapo dunia inakumbwa na misukusuko mingi, karate ni mbinu kubwa ya kujihami.