Alex kwenda QPR

Alex
Image caption Alex kuhamia kwa mahasimu wa Chelsea

QPR wamekubaliana bei na mahasimu wao wa magharibi mwa London Chelsea kumsajili beki kutoka Brazil Alex, BBC Sport inafamu.

Beki huyo wa kati, 29, alikuwa akisakwa na klabu ya Ligi Kuu ya England ambayo haikutajwa - ambayo ilidhaniwa kuwa QPR - mapema wiki hii.

Chelsea walikataa ombi hilo lakini wako tayari kuchukua ada ya uhamisho kwa mchezaji ambaye ameambiwa hana nafasi kubwa ya kucheza katika klabu hiyo baada ya yeye mwenyewe kuwasilisha maombi ya uhamisho.

Alex anatarajiwa kuanza mazungumzo na QPR wiki ijayo.

Hata hivyo mchezaji huyo alihusishwa na taarifa za kutaka kurejea kwao Brazil au kwenda kucheza soka Ufaransa.

Alex alisajiliwa na Chelsea kutoka PSV mwaka 2004, lakini alirudishwa Uholanzi kucheza kwa mkopo kutokana na matatizo ya kibali cha kucheza England, na alirejea mwaka 2007.

Wakati huohuo, Chelsea wako karibu kumsajili Gary Cahill kutoka Bolton kuchukua nafasi ya Alex, kwa mujibu wa BBC Sport.

Inaaminika kuwa beki huyo wa kati tayari amekubaliana maslahi binafsi na yuko London kwa ajili ya vipimo vya afya.