Uuzaji wa tiketi kuanza tena

Olympic Haki miliki ya picha
Image caption Michuano ya Olimpiki inasubiriwa kwa hamu

London 2012 imesema mfumo wake wa uuzaji tiketi za michuano ya Olimpiki wa mara ya pili utaanza tena hivi karibuni.

Lakini kampuni ya uuzaji tiketi ya Locog, ambayo ilisitisha uuzaji wa tiketi hizo Januari 6 baada ya matatizo ya kiufundi, haijasema hasa ni lini mfumo huo utaanza tena kupitia mtandao.

"Tumepata suluhu... ambayo itatoa huduma salama kwa watu kuuza tiketi zao," wamesema waandaaji.

Mchakato huo ulikusudiwa kuruhusu watu kujaribu kuuza tiketi zao wasizozitaka za michuano ya Olimpiki na Paralimpiki.

Locog haikuthibitisha kwamba wakati mfumo huo unafanya kazi, watu watakuwa pia na uwezo wa kununua tiketi kutoka katika wavuti huo katika kipindi hicho hicho.

Mfumo huo unaendeshwa na Ticketmaster na hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.

wale wote walionunua tiketi moja kwa moja kutoka kwa waandaaji wa michezo hiyo Locog, watakuwa na uwezo wa kuwasilisha tiketi zao kwa ajili ya kuuzwa tena katika wavuti huo hadi Februari 3.

Shughuli ya uuzaji tena wa tiketi ulianza Januari 6 lakini kulitokea matatizo kwa sababu wavuti huo ulikuwa na kasi ndogo na hivyo ukurasa huo kufungwa siku hiyo hiyo.

Kwa mfano tiketi zilizotangazwa za mpira wa mikono kwa wanaume katika nusu fainali zilipowekwa. Tiketi hizo zilinunuliwa mara tu zilipowekwa, lakini saa kadhaa baadaye tiketi hizo hizo zilikuwa zikionesha kuwa bado zipo.

Baadhi ya watu waliripoti kuwa walichagua tiketi lakini zilipotea muda mfupi kabla ya kuzilipia.

Januari 9 Locog ilifungua sehemu ya ukurasa wake na kuuza tiketi za kandanda na Paralimpiki. Inafuatia mfululizo wa matatizo ya uuzaji tiketi kwa Logoc. Mauzo ya kwanza yalilazimika kuongezwa muda baada ya ukurasa wa wavuti kuwa na kasi ndogo.

Katika raundi ya pili ya mauzo, maelfu ya watu walidhani wamenunua tiketi. Hata hivyo siku ya pili waliambia watarejeshewa fedha zao kwa kuwa hawakuwa wamenunua tiketi.

Maelfu ya tiketi za mchezo wa kuogelea zilitangazwa kuuzwa, ingawa hata kiuhakika hazikuwepo, na wateja walilazimika kubadilishiwa na kupewa tiketi ambazo wengi wanazisaka kama za fainali ya mbio za mita 100 za wanaume.

Kutakuwa na nafasi nyingine ya kuuza tiketi kuanzia Aprili 2012.