Anichebe hatimaye apata goli

Victor Anichebe
Image caption Mshambulizi kutoka Nigeria

Victor Anichebe siku ya Jumapili alifanikiwa kufunga goli, baada ya ukame wa zaidi ya miezi 22.

Everton ilifanikiwa kupata bao moja la ushindi, katika dakika za mwishomwisho dhidi ya West Brom.

Mechi hiyo ilielekea kumalizika kwa kutofungana mabao, hadi pale Anichebe alipoweza kuuvizia mpira baada ya kupigwa kwa kichwa kwa njia isiyokuwa ya kuridhisha kutoka kwa Paul Scharner katika dakika ya 87, na mkwaju huo kumpita mlinda lango Ben Foster.

West Brom, ambao pia wanajulikana kwa jina la utani kama 'Baggies', kabisa walishindwa kumshambulia vilivyo kipa Tim Howard, licha ya Peter Odemwingie wakati mmoja kukaribia kuimarisha juhudi hizo, lakini mpira ukapaa juujuu.