Sandro na Gallas majeruhi Tottenham

Harry Redknapp akabiliwa na majerhi wawili
Image caption Harry Redknapp akabiliwa na majerhi wawili

Tottenham inakabiliwa na tatizo la majeruhi licha ya kuilaza West Brom bao 1-0 baada ya kiungo wake Sandro na mlinzi William Gallas kutoka nje ya uwanja wakiwa wanachechemea baada ya kuumia mvungu wa paja.

"Sandro ameumia paja na inaelelekea itamchukua mrefu kupona," alibainisha meneja wa Spurs Harry Redknapp. "Gallas inaelekea na yeye pia ameumia mvungu wa paja. Watafanyiwa uchunguzi siku ya Jumatano."

Redknapp pia amesema alilazimika kumtoa nje Jake Livermore, ambaye alichanika mdomo alipogongana na mwenzake Younes Kaboul.

Wote wawili walilazimika kutibiwa nje ya uwanja.

Tukio hilo likaicha Spurs ikiwa na wachezaji tisa uwanjani kwa muda mfupi.

Licha ya matatizo hayo ambapo pia kwa sasa viungo wawili Scott Parker na Aaron Lennon tayari wameumia, kikosi hicho cha Redknapp kilifanikiwa kupata ushindi dhidi ya West Brom kwa bao lililofungwa kipindi cha pili na Jermain Defoe.

Kwa matokeo hayo Spurs imeendelea kujizatiti nafasi ya tatu ikiwapumulia kwa karibu Manchester City na United wakiwa na pointi 42.

Na Redknapp amesisitiza Defoe ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa England, akiwa ameanza kucheza tangu mwanzo mara ya kwanza kwa muda mrefu msimu huu, bado ni mchezaji muhimu katika kikosi chake.