Tottenham sambamba na Man.U

Luka Modric Haki miliki ya picha 1
Image caption Luka Modric

Ushindi wa Tottenham wa 2-0 dhidi ya Everton siku ya jumatano una maanisha wako sawa kwa pointi na bingwa mtetezi Manchester United na nyuma ya Manchester City kwa pointi tatu, na hilo bila shaka linaipa klabu hio na viongozi wake matumaini ya kushindania ubingwa wa Ligi kuu.

Mwezi mmoja tu uliopita, mchuano wa nani anayeweza kua bingwa wa Ligi kuu ya England ulikua baina ya City na Manchester United kileleni. Lakini tangu hapo pande hizi zote zimepoteza pointi na hali nzuri ya Tottenham kuzidisha presha dhidi ya vilabu hivyo.

Hakuna mtu yeyote aliyeidhania Spurs kuweza kupaa hadi hapa ilipo hata kufikia nne bora msimu huu, lakini hio ni kwa sababu ya sintofahamu iliyokuepo juu ya mcheza kiungo Luka Modric kama atabaki kuichezea klabu hio au la.

Lau kama Modric angeuzwa kwa Chelsea iliyomtamani mnamo mwezi Agosti, hivyo klabu hio ingehesabiwa kama ya biashara ya kuuza wachezaji wake mahiri na kua mwaliko kwa wanaotaka wachezaji waje wajizolee.

Hali hio ya kutakikana na klabu kama Chelsea yenye uwezo wa kumlipa Modric mshahara mkubwa kuliko Tottenham ingeweza kumchanganya mchezaji huyo na kumkosesha raha na hivyo kiwango chake kushuka, lakini Modric hakubadilika na sasa msimamo wa kocha wake wa kutomuuza umezaa matunda.

Pamoja na kumkatalia Modric, usajili wa Harry Redknapp ulikua mzuri ukiwaleta wachezaji kama Scott Parker katika kiungo na mshambhuliaji Emmanuel Adebayor pamoja na mkongwe katika goli Brad Friedel.

Mbali na hadithi hio, kwa sasa klabu hio inapitia kipindi cha kujivunia. Katika majuma machache yaliyopita klabu hio imekua ikicheza soka ya kupendeza pamoja na kutoa matokeo ya kuridhisha kuliko klabu nyingine yoyote.

Ikiwa wanaweza kuendelea na hali kama hio kupitia kipindi cha Msimu kilichosalia, basi ndoto ya mashabiki, Kocha Harry Redknap na Mwenyekiti Daniel Levy ya kumalizia kwa ushindi wa Ligi kuu.

Lakini kabla ya kububujika na furaha ya kupindukia Tottenham inakaribia kupewa majaribio makali kama itaweza kuendelea kupaa. Kuanzia Jumapili tareh 22 Januari, ina mchuano mkali na Manchester City, kisha Liverpool, Arsenal na Manchester United katika kipindi cha majuma sita.

Mtihani mwingine ni jumamosi hii tarehe 14 Spurs itakapochuana na Wolverhampton Wanderers ambayo mbali na kushiriki Ligi kuu, ni kama mfa maji ikipania kutoshuka daraja msimu ujao, kwa hio ni pambano la kufa na kupona kwao.