Wanyama mchezaji bora wa mwezi Scotland

Wanyama
Image caption Lennon amekuwa akitegemea huduma za kiungo Victor Wanyama

Victor Wanyama kutoka Kenya anayechezea Celtic ametajwa kuwa mchezaji bora kijana wa mwezi katika ligi kuu ya Scotland.

Meneja wake Neil Lennon naye ametajwa kuwa meneja bora wa mwezi Disemba.

Celtic imekuwa na mafanikio katika mwezi uliopita baada ya kushinda mechi zake tano za ligi na kukaa kileleni mwa ligi wakiwa pointi mbili zaidi kuliko klabu iliyo nafasi ya pili.

Ushindi dhidi ya Dundee United na Hearts ulifuatiwa na ushindi mwingine dhidi ya St Johnstone na Kilmarnock.

Celtic ilimaliza mwezi Disemba kwa kuwachapa mahasimu wao Rangers kwa 1-0.

Kwa mwezi mzima, Wanyama, 20, alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Lennon, na hata kufunga katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Hearts.

Raia huyo wa Kenya aliwasili Celtic akitokea klabu ya Germinal Beerschot ya Ubelgiji kwa uhamisho wa fedha ambao haukutajwa, mwezi Julai mwaka jana kwa mkataba wa miaka minne.