Ndoto za Olimpiki katika picha

Imebadilishwa: 16 Januari, 2012 - Saa 20:33 GMT

Ndoto za Olimpiki

 • Usain Bolt, mwanariadha kutoka Jamaica na anatazamiwa kufanya maajabu 2012

  "Mimi sio 'mkongwe' bado. Naelekea huko, lakini nahitaji kwenda London na kuwafurahisha watu."

  Usain Bolt ni mmoja wa wanariadha machachari duniani ambaye anafuatiliwa kwa karibu na BBC wakatiwakijiandaa na michuano ya Olimpiki ya London 2012. Je wamefanikiwa kiasi gani mwaka 2011? Ushindi wa kishindo sio kitu ambacho Usain Bolt atasema atajivunia mwaka 2011. Alitolewa katika fainali ya mita 100 ya michuano ya dunia kwa kuanza kabla ya wenzake. Hata hivyo alitetea ubingwa wake wa mita 200 na kuweka rekodi mpya na timu ya mbio za vijiti za mita 4x100. Alimaliza msimu kwa muda wake wa kasi katika mita 100 kwa sekunde 9.6 mjini brussels, Ubelgiji.

 • Nadel el Masri, mkimbiaji wa mbio ndefu kutoka Gaza na anatarajia kushiriki Olimpiki Lomdon 2012

  "Nina kocha lakini hakuna aliye kwenye kiwango changu Gaza. Nalazimika kufanya mazoezi yangu peke yangu"

  Nadel el Masri, mkimbiaji wa mbio ndefu kutoka Gaza na anatarajia kushiriki Olimpiki Lomdon 2012

  El Masri alithibitishwa kuwa ni mwanariadha mahiri, wakati aliposhinda mbio za kwanza kuwahi kufanyika Gaza. Mpalestina huyo amekimbia muda wake mzuri wa dakika 14 na sekunde 21 katika mita 5,000 - wakati muda wa kufuzu Olimpiki ni dakika kumi na tatu na sekunde 27. El Masri ameambiwa hatopewa nafasi ya kufuzu bila kufikia kiwango katika michuano ya 2012.

 • Alistair Brownlee, Mwingereza Bingwa mara mbili wa dunia wa triathlon na anatarajiwa kushiriki Olimpiki London 2012

  "Ilikuwa kweli, kweli siku muhimu kwangu kuwa bingwa wa dunia mara mbili! si watu wengi wanaweza kusema hivyo"

  Alistair Brownlee, Mwingereza Bingwa mara mbili wa dunia wa triathlon na anatarajiwa kushiriki Olimpiki London 2012

  Alistair alivishwa taji la dunia mwezi Septemba, na kuongeza taji la dunia aliloshinda mwaka 2009. alimaliza mwaka wake vyema baada ya kutetea ubingwa wa Ulaya nchini Uhispania na pia kufuzu michuano ya London 2012 baada ya kushinda michuano ya Hyde Park triathlon.

 • Haider Rashid, mpiga makasia kutoka Iraq na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Nitafanya kila niwezavyo kufuzu kwa sababu nahitaji kufanya hivyo"

  Haider Rashid, mpiga makasia kutoka Iraq na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Haider Rashid alimwambia Matthew Pinsent katika michuano ya dunia ya kupiga makasia nchini Slovenia kuwa lengo lake kwa mwaka 2011 ni kufuzu kushiriki Olimpiki ya London 2012. Rashid alimaliza katika nafasi ya 27 kati ya washiriki 34 upande wa wanaume, na bado ana nafasi ya kufuzu kupitia mchujo wa Asia utakaofanyika Aprili 2012.

 • Olga Kharlan, mcheza fensi wa Olimpiki kutoka Ukraine

  "Bibi yangu anasema tayari nina kila kitu ambacho wao hawakuwahi kuwa nacho maisha yao yote"

  Olga Kharlan, mcheza fensi wa Olimpiki kutoka Ukraine

  Ulikuwa mwaka ambao Olga alitawala Ulaya na almanusura atawale dunia. Alishinda ubingwa wa Ulaya mjini Sheffield lakini aliambulia medali ya shaba katika michuano ya dunia nchini Italia. Kibinafsi, ameshinda na kupata kipato cha kujenga nyumba yake na kuweza kuhama katika nyumba ndogo ya wazazi wake.

 • Julien Absalon, mwendesha baiskeli wa Ufaransa na mtarajiwa wa Olimpiki London 2012

  Julien Absalon, mwendesha baiskeli wa Ufaransa na mtarajiwa wa Olimpiki London 2012

  Mfaransa huyu mara nyingi hutawala michuani ya nyika ya dunia lakini mwaka 2011 alifanikiwa tu kupata mdedali ya fedha katika michuano ya Ulaya na shaba katika michuano ya dunia. Hata hivyo ametawazwa kuwa bingwa wa Ufaransa kwa mara ya tisa na pia alishinda michuano ya London Olympic Test 2012 iliyofanyika Hadleigh Farm, Essex nchini Uingereza.

 • Majlinda Kelmendi, mcheza judo kutoka Kosovo na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Nimekataa wito kutoka nchi kadhaa kubwa, lakini naiwakilisha Kosovo na sitaki mtu aniambie kwamba haiwezekani"

  Majlinda Kelmendi, mcheza judo kutoka Kosovo na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Kufuzu kushiriki London 2012 kulihakikishwa mwezi Oktoba wakati Majlinda aliponyakua medali tatu za dhahabu katika muwa wa wiki tatu. Mafanikio yake yalimpandisha hadi katika nafasi ya tatu katika msimamo wa dunia wa mchezo wa judo katika utizo wa kilo 52. Mwaka 2012 Majlinda ana matumaini ya kuwa mwanamichezo wa kwanza kuiwakilisha Kosovo katika Olimpiki - jambo gumu ukizingatia nchi hiyo haitambuliwi rasmi ya Kamati yya Olimpiki ya Kimataifa IOC.

 • Jehue Gordon, mwanariadha kuruka viunzi kutoka Trinidad na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Hauhitaji kujizuia kutokana na hali uliyonayo. Kwa sababu unatokea geto haimaanishi uwe na tabia za kigeto."

  Jehue Gordon, mwanariadha kuruka viunzi kutoka Trinidad na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Katika mbio za Diamond League mwezi Mey, Jehue alikimbia kwa muda wa sekunde 49.09, muda wa kutosha wa kufuzu kushiriki Olimpiki ya London. Alisikitika wakati aliposhindwa kufuzu kukimbia fainali ya mita 400 katika michuano ya dunia kwa kukosa moja ya mia moja ya sekunde. Wiki moja na nusu baadaye aliweka muda mzuri binafsi wa sekunde 48.66 - muda wa kasi wa 13 mwaka 2011.

 • Linet Masai, mkimbiaji wa mbio ndefu kutoka Kenya na mtarajiwa wa Olimpiki London 2012

  Linet Masai, mkimbiaji wa mbio ndefu kutoka Kenya na mtarajiwa wa Olimpiki London 2012

  Linet alianza mwaka kwa kushinda mbio za Great Winter mjini Edinburgh, Scotland. Alimaliza sekunde nane mbele ya mwenzake Vivian Cheruiyot, ambaye alilipiza kisasi kwa kumshinda katika michuano ya dunia ya nyika - kwa mara ya tatu mfululizo Linet alimaliza wa pili. Aliweza kutetea taji lake la New York la kilomita 10, lakini katika michuano ya dunia ya Korea, alishindwa na Vivian Cheruiyot ambaye alinyakua taji la Linet la mita 10,000.

 • Luol Deng, mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka Uingereza na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Nimefurahi sana kuwa tuko wote hapa, kila mtu aliyekimbia. Nimefurahi kuwa hata wazazi wangu wameweza kushuhudia siku hii ya leo. Kila walichojitolea kimetufaa."

  Luol Deng, mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka Uingereza na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Luol Deng atashiriki katika michuano ya London 2012 baada ya Fiba, shirikisho la mchezo huo la dunia, kuipa timu ya Uingereza ruhusa ya kushiriki.Na baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa kimataifa wa mwaka na chama cha waandishi wa habari wa Uingereza, Luol Deng alikuwa alikuwa mchezaji nyota wa timu ya Uingereza katika michuano ya Ulaya ya mpira wa kikapu. Mbali na michezo, Luol pia alizuru Sudan Kusini kwa mara ya kwanza tangu alipokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati wakiwa mtoto.

 • MC Mary Kom, bondia wa India na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London

  "Ulikuwa uamuzi wa mgumu kwake kuondoka kabla ya upasuaji wa mtoto wetu wa kiume, lakini aliniahidi kuwa atachukua nafasi ya kwanza, na nimefurahi alifanya hivyo." Omler Kom

  MC Mary Kom, bondia wa India na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London

  Bondia huyo mwenye mwili mdogo kutoka Manipur amelazimika kuganwanya muda wake kufanya mazoezi na kuhmhudumia mwanaye mmoja ambaye ni mgonjwa. Wakati mwanae anaandaliwa kupelekwa kufanyiwa upasuaji wa moyo, Mary Kom alinyakua kombe la Asia kabla ya kushinda taji la nane la ubingwa wa India katika kipindi cha miaka 12. Mwezi Novemba alihudhuria majaribio ya Olimpiki na kuzua utata kuhusu mabondia wa kike kwa kusema wanalazimishwa kuvaa sketi, akisema: "Wacheza tennis wanavaa sketi, wacheza badminton wanavaa sketi, kwa nini mabondia wasivae pia sketi?"

 • Merlin Diamond, mkimbiaji kutoka Namibia na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Ukitafuta maisha mazuri na unataka kupata mazuri kutokana na unachofanya, inabidi utoke na ujitolee katika mambo mengi."

  Merlin Diamond, mkimbiaji kutoka Namibia na mtarajiwa katika michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Mwaka 2011 kwa Merlin Diamond haukuwa wenye mn'garo sana. Mwanzo mwa mwaka alikwenda Uingereza kwa mara ya kwanza kuutazama uwanja wa Olympic Park mashariki mwa London. Baadaye aliwaacha ndugu zake na marafiki na kuhudhuria mazoezi ya hali ya juu katika kisiwa cha Mauritius. Ingawa alikuwa na bahati kwa kudhaminiwa na IOC, vifaa vilikuwa duni na akapatwa na msongo wa mawazo. Aliporejea Namibia alikuwa amenenepa na akishindwa hata kukimbia na kuweza kufuzu London 2012.

 • Rohullah Nikpai, mchezaji wa taekwondo kutoka Afghanistan na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Kupitia kushinda medali nina imani ya kuleta amani na maelewano katika nchi"

  Rohullah Nikpai, mchezaji wa taekwondo kutoka Afghanistan na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Mshindi pekee wa medali ya Olimpiki kutoka Afghanistan yuko tayari kusaka medali nyingine 2012. Rohullah alifuzu kushiriki London 2012 kwa kunyakua medali ya shaba katika uzito wa kilo 68 katika michuano ya kufuzu ya Olimpiki mjini Bangkok, Thailand. Hii ilifuatiwa na medali ya shaba aliyoshinda mwezi Mei katika michuano ya dunia ya taekwondo nchini Korea Kusini.

 • Shawn Johnson, mwanasarakasi kutoka Marekani na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Mimi kuchaguliwa, ilisababisha nikatoa machozi. Kurejea katika timu ni jambo muhimu kwangu. Nilikuwa nikisema, ni majaribio tu, lakini sasa imekuwa kweli."

  Shawn Johnson, mwanasarakasi kutoka Marekani na mtarajiwa wa michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Baada ya kuumia goti katika ajali ya mchezo wa kuteleza kwenye barafu mwaka 2010, Shawn Johnson alipigana kufa na kupona kurejea katika timu ya sarakasi wa Marekani mwaka 2011. kwa bahati mbaya hakuchaguliwa katika michuano ya dunia ya sarakasi mjini Tokyo. Badala yake, alishinda medali mbili katika michuano ya Pan American. Kampuni ya Nike ilionesha imani yake kwa mwanamichezo huyo kwa kumpa udhamini na sasa ana hadi mwezi Juni kujiandaa kwa ajili ya timu ya Marekani ya Olimpiki katika majaribio mjini San Jose.

 • Wu Minxia, mchupaji kutoka Uchina na mtarajiwa wa Michuano ya Olimpiki ya London 2012

  "Mimi ndio msichana mwenye umri mkubwa zaidi katika timu, kwa hiyo nina majukumu kama ya dada na timu yote wananiita dada Xia."

  Wu Minxia, mchupaji kutoka Uchina na mtarajiwa wa Michuano ya Olimpiki ya London 2012

  Wu Minxia na mchupaji mwenzake He Zi walishinda mara nne michuano ya dunia kabla ya kufuzu kucheza London 2012. Kila walichofanya kiliwapatia dhahabu na walitawala michuano ya dunia mjini Shanghai kwa mara ya kwanza wakicheza pamoja. Hata hivyo ilikuwa ni dhahabu ya michuano ya kuchupa majini nchini Uhcina mwezi Septemba ndio iliwapatia nafasi ya kufuzu kwa ajili ya michuano ya London. Tangu 'malkia wa kuchupa' Guo Jingjing alipostaafu, Wu amekuwa ndio kinara wa Uchina katika kuchupa, chama cha kuogelea kilimtunuku tuzo ya mchupaji bora wa kike wa mwaka.

This is a test include:

Bofya kwenye picha au mwaka
 • Ujerumani
 • Timu za Uingereza
 • Afrika
 • Tafuta timu

Viwango

 • 1930
 • 1934
 • 1938
 • 1950
 • 1954
 • 1958
 • 1962
 • 1966
 • 1970
 • 1974
 • 1978
 • 1982
 • 1986
 • 1990
 • 1994
 • 1998
 • 2002
 • 2006
 • 2010
Linganisha timu
Futa yote
Chagua zote

  • 1930
  • 1934
  • 1938
  • 1950
  • 1954
  • 1958
  • 1962
  • 1966
  • 1970
  • 1974
  • 1978
  • 1982
  • 1986
  • 1990
  • 1994
  • 1998
  • 2002
  • 2006
  • 2010

  Brazil ni timu pekee ambayo imekuwa ikicheza fainali zote za Kombe la Dunia. Imeshinda ubingwa kwa mara kwanza mwaka 1958 wakati Pele akiwa kijana akipachika magoli mawili siku ya fainali. Kwa kutumia mfumo wetu wa magolil, ilimaliza ikiwa miongoni mwa timu za juuu mwaka 1950 katika mashindano ambayo yalikubwa na matukio ya baadhi ya mataifa kujitoa. Bingwa halisi fainali hizo kwa wakati huo ilikuwa ni nchi ya Uruguay.

  Ujerumani

  Mshindani mkubwa wa mara kwa mara wa Brazil katika mashindano hayo ya Kombe la Dunia ni timu ya taifa ya Ujerumani. Timu hizi zote zimekuwa zikimalizia nafasi ya nane kila mwaka kuanzia mwaka 1950, wakati nchi hiyo ikiwa bado kwenye vita ambapo ilikuwa imezuiwa kushiriki mashindano. Ujerumani imeshinda mashindano hayo ya Kombe la Dunia mara tatu, ikiwemo mwaka 1974 japokuwa kwenye kumbukumbu zetu kwenye jedwali Poland ilikuja juuukwa mwaka huo kwa tofauti ya magoli.

  Timu za Uingereza

  England ni timu pekee iliyoshinda Kombe la Dunia ikiwa nyumbani na imekuwa na rekondi nzuri ambapo mara kwa mara imekuwa ikimaliza katika kumi bora. Scotland imekuwa taratibu ikishuka lakini timu zote za nyumbani zimekuwa zikijitahidi hasa zinapokuwa zikishiriki mashindano makubwa ya dunia. Ni mwaka wa 1958 pekee ilipotoa timu zote za mataifa manne ya Uingereza ikiwa ni pamoja na Wales kufikia hatua ya fainali hadi leo huku Ireland ikimaliza katika ya timu nane bora.

  Afrika

  Aliyewahi kuwa mchezaji bora mara tatu, Pele alitabiri kuwa timu ya kiafrika ingeshinda mashindano ya kombe la dunia kabla ya mwaka 2000, lakini hakuna timu ya kiafrika ambayo imefanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali, hata hivyo karibu timu zote zilionesha jitihada katika kipindi cha karne iliyopita.Cameroon imeweka rekodi ya kuingia katika michuano ya kombe la dunia lakini bado haijafanikiwa kufanya vyema kama ilivyokuwa mwaka 1990 ambapo magoli ya Roger Milla yaliwafurahisha wengi.

  2010: Mwenyeji ilikuwa Afrika Kusini, Bingwa ilikuwa Hispania

  • England walidhalilishwa na Ujerumani baada ya kuzabwa mabao 4 - 1 katika timu 16 za mwisho baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Marekani katika hatua za makundi, ambapo timu hiyo iliyokuwa chini ya kocha Fabio Capello ilitoka sare ya kufungana bao 1 - 1, na 0 - 0 na Algeria kabla ya kuifunga Slovenia kwa 1 -0.
  • Mshangao mkubwa ilikuwa pale timu ya Uswis ilipoifunga Hispania bao 1-0 katika mashindano ya ligi ya Ulaya,lakini Uswis hao hao wakashindwa kwa bao 1 dhidi ya Chile na kisha kutoa sare ya 0-0 dhidi ya Honduras
  • Italia imemaliza mashindano katika kundi lao kwa kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Paraguay na New Zeland baada ya kufungwa magoli 3-2 na Slovakia wakati ambapo Ufaransa pia ilipoteza mchezo na Mexico baada ya kufungwa 2-0 huku mwenyeji Afrika kusini wakifungwa mabao 2-1 dhidi ya Italia katika na hivyo kuondolewa mapema
  • Uholanzi iliifunga Brazil 2-1 katika mchuano wa robo fainali na Uruguay 3-2 katika hatua ya nusu fainali, wakati Uhispania iliishinda Ujerumani kwa bao 1-0 katika hatua ya nusu fainali kabla ya kushinda kwa mara ya kwanza michuano ya kombe la dunia kwa kuifunga Uholanzi bao 1-0 katika muda wa nyongeza.

  2006: Mwenyeji ilikuwa Ujerumani, Bingwa ikawa Italia

  • England ilisonga mbele katika hatua ya makunbdi bila kufungwa wakati iliposhinda 1 - 0 dhidi ya Paraguay na kuifunga Trinidad na Tobago 2 - 0 kabla ya kutoka sare ya 2 - 2 na Sweden. Iliifunga Ecuador 1 - 0 ushindi uliokuja baada ya timu aliyokuwa ikifundishwa na Sven-Goran Eriksson kufungwa na Ureno kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya robo fainali. England ilicheza na wachezaji 10 kufuatia kuondolewa kwa kadi nyekundu Wayne Rooney.
  • Yalikuwa mashindano yenye kusisimua wakati michuano ilipokutanisha washindi sita wa zamani katika hatua ya robo fainali ambapo ufaransa iliifunga Brazil kwa bao 1-0 huku timu wenyeji, ujerumani ikiiondoa Argentina katika hatua ya penati.
  • Timu nne zilizobaki kutoka bara la ulaya zilikutana katika nusu fainali huku Italia ikiifunga Ujerumani mabao 2-0 katika muda wa nyongeza, kabla ya ufaransa kuiondoa ureno kwa bao 1-0.
  • Italia ilishinda fainali kwa mikwaju ya penalti, lakini kabla ya mchezeji mkongwe wa Ufaransa kiungo Zinedine Zidane hajatolewa kwa kadi nyekundu katika dakika za nyongeza kwa kumpiga kichwa kwenye kifua mchezaji wa Italia Marco Materazzi.

  2002: Mwenyeji ilikuwa ni Japan na Korea Kusini na bingwa ilikuwa ni Brazili

  • Uingereza ilipiga hatua baada ya kuifunga Argentina kwa bao 1-0 katika hatua ya makundi na kutoka sare ya 1-1 na Sweden na kutoka suluhu ya kutofungana na Nigeria.England chini ya Kocha wao Sven-Goran Eriksson, iliibamiza Denmark kwa mabao 3-0 kabla ya kuondolewa katika hatua ya robo fainali na Brazil kwa kufungwa magoli 2-1, ambapo mpira wa adhabu wa Ronaldinho ulileta madhara kwa Mlinda mlango David Seaman
  • Jamuhuri ya Ireland alifuzu kusonga mbele katika hatua ya makundi bila kufungwa ambapo ilitoka sare ya 1 - 1 na Cameroon na Ujerumani kabla ya kuifunga Saudi Arabia 3 - 0. Robbie Keane katika dakika ya 90 akaisaidia kuingia na Hispania katika hatua ya kupigiana mikwaju ya penalti kwenye mzunguko unaofuata ambapo ilifungwa kwa penati 3 - 2.
  • Tangu Senegal iliposhinda goli 1 - 0 dhidi ya Bingwa mtetezi Ufaransa wakati wa mechi ya ufunguzi Korea Kusini ilifanikiwa kufikia nusu fainali baada ya ushindi dhidi ya Italia 2 - 1 na Hispania kwa penalti 5 - 3 ambapo yalikuwa ni mashindano ya matokeo ya kushtua.
  • Hatimaye Ujerumani ikaizamisha Korea baada ya kushinda 1 - 0 ambapo upande wa Rudi Vollers ulifungwa na Brazil magoli 2 - 0 katika mechi ya fainali ambapo Ronaldo alishinda kiatu cha dhahabu kwa kufunga magoli yote na kuchukua kombe la dunia kwa mara ya nane. Uturuki ikishangaza kwa kumaliza ikishika nafasi ya tatu.

  1998: Mwenyeji ilikuwa Ufaransa na Bingwa ikiwa pia Ufaransa

  • Scotland kwa mara ya mwisho iliondolewa kwenye hatua ya makundi kwa magoli 2 - 1
  • Kikosi cha England chini ya ukufunzi wa Glenn Hoddle,kilitolewa na Argentina kwa mikwaju ya Penalt katika hatua ya kumi na sita bora,katika mechi iliyoamriwa kwa mikwaju ya Penalt baada ya kumalizika muda wa ziada timu hizo zikiwa sare ya bao 2-2.Kijana Michael Owen alitangulia kufunga goli murua kwa juhudi zake binafsi baada ya kuwalamba chenga walinzi kadhaa wa Argentina,kabla ya David Beckham kutolewa kwa kadi nyekundu.Katika mechi za makundi England iliilaza Tunisia 2-0,wakafungwa 2-1 na Romania kabla ya kuilaza Colombia 2-0.
  • Hispania walishindwa kuvuka hatua ya makundi baada ya kuchapwa bao 3-2 na Nigeria,huku Croatia wakiwashangaza wengi kwa kutinga hadi nusu Fainali baada ya kuilaza Ujerumani bao 3-0 katika mechi ya Robo Fainali.
  • Wenyeji Ufaransa waliowachapa Italia kwa mikwaju ya Penalt kwenye Robo Fainali,walihitimisha safari ya Croatia kwa kuilaza bao 2-1 katika mechi ya nusu Fainali,Kabla ya kuhitimisha Michuano hiyo kwa kuilaza Brazil bao 3-0 kwenye mechi ya Fainali na kutwaa Ubingwa mechi iliyoshuhudia Zinedine Zidane akifunga mara mbili.

  1994: Mwenyeji ilikuwa ni USA Bingwa akawa Brazil

  • Wakati England ilishindwa kufuzu, Jamuhuri ya Ireland ilichukua nafasi na kuishtua Italia kwa kuifunga goli 1 - 0 katika mechi ya ufunguzi kabla ya kufungwa na Mexico 2 - 1 na kutoka sare ya 0 - 0 na Norway. Ilimaliza mashindano katika hatua ya 16 wakati ilipofungwa 2 - 0 na Netherlands.
  • Bulgaria ilisaidiwa na Hristo Stoichkov magoli sita wakati ambapo mashindano yaliposhangaza hasa wakati walipoifunga Argentina magoli 2 - 0 katika hatua ya makundi, na kuifunga Mexico kwa penalti katika mzunguko wa pili na kuifunga Ujerumani kwa magoli 2 - 1 katika hatua ya nane bora. Romania pia iling'ara baada ya kuifunga Argentina 3 - 2 katika hatua ya mtoano kabla ya kufungwa na Sweden kwa mikwaju ya penalti katika hatua robo fainali.
  • Brazil ikiwa na wambuliaji pacha Romario na Bebeto waliifunga Urusi 2 - 0 na Cameroon 3 -0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza, kabla ya kuondoa Marekani kwa goli 1 - 0 na kuiadhibu Netherland kwa magoli 3 -2 na Sweden 1 -0. Italia nayo ikaingia fainali kwa kuifunga Norway 1 - 0, Nigeria 2 -1, Hispania 2 -1 na Bulgaria 2 -1 katika hatua ya nusu fainali.
  • Brazil ilinyakua Kombe la Dunia kwa kuifunga Italia kwa mikwaju ya penalti baada kutofungana katika mechi ya fainali. Roberto Baggio alikosa penalti muhimu ya kuamua Bingwa.

  1990: Mwenyeji Italia, Bingwa Ujerumani Magharibi

  • England ikiwa kwenye kiwango cha ubora tangu ilipotwaa Kombe la Dunia mwaka 1966,baada ya kuanza kwa mwendo wa taratibu kwa kwenda sare na Jamhuri ya Ireland na Uholanzi,waliweza kuilaza Misri bao 1-0 na kisha wakasonga mbele kwenye hatua ya mtoano ambapo waliiza Ubelgiji bao1-0,kisha Camerounn bao3-2 huku mechi zote zikiamriwa katika muda wa ziada.Katika Mechi iliyojaa msisimko ya Nusu Fainali iliyoshuhudiwa Mchezaji mahiri Paul Gascoigne akibubujikwa machozi baada ya kupewa kadi ya njano ambayo ingemzuwia kucheza mechi ya Fainali.England hatimaye walitolewa na Ujerumani bao 4-3 kwa mikwaju ya penalt baada ya kumaliza muda wa ziada matokeo yakiwa sare 1-1.
  • Jamhuri ya Ireland imeweka rekodi ya sare tatu mfululizo katika kundi lake dhidi ya timu ya taifa ya England ,Misri na Netherlands, kabla ya kutembeza kipigo cha 5-4 dhidi ya Romania katika mzunguko wa mwisho ambapo walitolewa katika robo fainali baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya mwenyeji wao Italy.Scotland pi ilifanikiwa kuvuka robo fainal, lakini pia ikashindwa kuvuka katika kundi hilo baada ya kufungwa na Costa Rica na kisha wakafungwa na Brazil mabao 2-1 dhidi Sweden
  • Cameroon iliushitua ulimwengu katika mashindano ya ufunguzi baada ya kuwafunga watetezi wa ubingwa huo Argentina,kabla ya kutembeza kipigo kingine cha 2-1 kwa Romania ikiwa ni matokeo ya jitihada za Roger Milla, ambapo waliendeleza ubabe huo katika hatua ya mtoano pale walipoichabanga Colombo 2-1 kabla ya kupoteza mchezo wake na England
  • Wenyeji Italia walipoteza panalt 4-3 dhidi ya Argentina katika nusu fainal,kabla ya ujeruman magharibi kuifunga Amerika ya Kusini 1-0 katika hatua ya fainali

  1986:Wenyeji Mexixo,washindi Argentina

  • Ushiriki wa Uingereza ulihitimishwa na Goli la Diego Maradona, lililodaiwa kuwa ni la mkono wa Mungu na ambalo lilihitimisha safari ya uingereza katika mashindano hayo katika robo fainali baada ya kufungwa 2-1 na Argentina.Uingereza pia katika mchezo wao wa ufunguzi walifungwa 1-0 dhidi ya Ureno,hata hivyo kocha Bobby Robson kabla ya kutolewa alikuwa ametoa sare na Morocco na kuzifunga Poland na Paraguay 3-0 ili kufikia nane bora
  • Scotland ilishindwa mechi yake dhidi ya Dernmark baada ya kuchabangwa 1-0,ikafungwa 2-1 dhidi ya Ujeruman Magharibi kabla ya kutoa sare na 0-0 na Uruguay.Halkadhalika Ireland Kaskazin walitoa sare 1-1 na Algeria,lakini ikafungwa 2-1 na Hispania na 3-0 na Brazil
  • Timu ya Belgium ilianza vizuri safari ya kuelekea nusu fainali,baada ya kuibwaga Urusi ya zaman 4-3 katika penalti 16 zilizopigwa na Hispania katika robo fainal kabla ya kufungwa 2-0 na Argentina katika nusu fainal
  • Ujeruman Magharibi walioishinda Ufaransa 2-0 katika nusu fainal,walikuwa ni Argentina ambao walifungwa mabao 3-2.Mfungaji Gary Lineker ndiye aliyeshinda kiatu cha dhahabu baada ya kujifungia jumla ya mabao 6

  1982:Mwenyeji Hispania,Mshindi Italia

  • Ireland ya kaskazini ni moja kati ya timu zilizosababisha mshangao baada ya kuwapiga wenyeji Hispania 1-0 katika hatua ya makundi,baada ya kutoa sare 1-1 dhidi Honduras na 0-0 na Yugoslavia, japo kuwa walitolewa katika mzunguko wa pili kwa sare ya mabao 2-2 na Austria na kufungwa magoli 4-1 na Ufaransa
  • Uingereza chini ya Ron Greenwood ilifanikiwa kushinda mizunguko yote mitatu ya awali dhidi ya Ufaransa 3-1,Czechoslavikia 2-0,na Kuwait 1-0 lakini ilitolewa katika kundi la pili kwa tofauti ya magolina Ujeruman Magharibi na Hispania.
  • Scotland haikuweza kumaliza mzunguko wa kwanza pamoja na kuanza kwa mafanikio katika mechi ya ufunguzi baada ya kuibwaga New zeland 5-2. hata hivyo wakapoteza mchezo wao wa pili baada ya kufungwa 4-1 na Brazil,na ilimaliza na sare ya 2-2 na Jamhuri ya Urusi
  • Washindi wa ligi ya Ulaya Ujeruman walitunukiwa mabao 2-1 na Algeria mwanzoni mwa ligi,lakini wakapata ahueni baada ya kuifunga Ufaransa kwa penalti katika nusu fainali,baada ya kumaliza mchezo wakiwana sare ya 3-3.na pia ikafungwa 3-1 na Italia katika fainali

  • Scotland ilikuwa ni timu pekee kuifikia Argentina mwaka 1978,lakini pia ikarejea nyumbani baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza.walianza kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Peru,sare 1-1 na Iran,na kisha kuifunga Netherlands 3-2 huku Archie Gemmil akifunga mara mbili
  • Kulikuwa na mishangao ya mapema,baad aya Austria kuifunga Hispania 2-1 na Swedeen 1-0 ushindi ulioifanya timu hiyo kuwa mbele ya Brazil.Peru ilimaliza mbele ya Netherlands, wakati Poland iliongoza kundi lake mbele ya Ujerumani
  • Ujerumani Magharibi walitolewa katika kundi la pili baada ya kutoa sare 0-0 na Italia,2-2 na Netherland na kisha wakafungwa na Austria 3-2
  • Netherlands,ambayo iliichapa Austria 5-1 na Italia 2-1 katika mzunguko wa pili,ilicheza na Argentina katika fainali lakini walishindwa kwa kipigo cha mabao 3-2 baada ya muda wa nyongeza, Mario Kempes alifunga mabao mawili kabla ya wenyeji wa mchezo huo kunyakua kombe.

  1974:mashindano yaliandaliwa na Ujerumani magharibi na nchi hiyo ikanyakua ubingwa

  • Uingereza ikiwa imeshindwa kufuzu, Scotland nayo iliondolewa katika mzunguko wa kwanza wa michuano ingawa haikuwahi kufungwa. walishinda 2-0 dhidi ya Zaire,suluhu ya kutofungana na Brazil na kutoka na Yugoslavia kwa bao 1-1
  • Wenyeji wa michuano Ujerumani Magharibi walimaliza wakiwa washindi wa pilli katika hatua ya makundi, wakipoteza mchezo baada ya kukabiliana na majirani zao ujerumani mashariki kwa kufungwa bao 1-0 ambayo pia waliifunga Australia 2-0 na kutoka sare ya 1-1 na Chile.Poland ilifanya vizuri katika awamu ya kwanza, baada ya kuifunga Argentina 3-2 na Italia 2-1.
  • timu nane zikiwa zimegawanyika mara mbili katika mzunguko wa pili,Netherlands na Ujerumani magharibi walifanikiwa kuingia fainali huku timu zote mbili zikiwa zimeshinda michezo mitatu.
  • Ujerumani magharibi iliichapa Netherlands kwa mabao 2-1,huku Poland ikiipiga Brazil 1-0 na kumaliza ikiwa nafasi ya tatu.

  Mexico iliongoza michuano mwaka 1970, ushindi ulichukuliwa na Brazil

  • wenyeji wa michuano, Uingereza iliongoza kwa 2-0 kisha kupoteza mchezo katika dakika za nyongeza baada kwa kufungwa 3-2 na Ujerumani magharibi katika mchuano wa robo fainali.Katika hatua ya awali ya makundi,Uingereza iliyoongozwa na Alf Ramsey iliifunga Romania bao 1-0 na Czechoslovakia 1-0,kisha kupoteza mbele ya Brazil kwa goli 1-0 kikosi kilichokuwa na mchezaji machachari, Pele.
  • Urusi ilifanya vizuri katika hatua ya makundi kwa kutoka suluhu na wenyeji, MExico,ikaichapa Belgium 4-1 na El Salvador 2-0, haa hivyo ilipoteza mchezo kwa kuchapwa goli 1-0 na Uruguay katika hatua ya robo fainali.
  • Italia ilionesha mchazo wa kuvutia katika hatua ya mtoano kwa kuichapa Mexico mabao 4-1 na ujermani magharibi 4-3 huku Brazil ikishinda mabao 4-2 dhidi ya Peru na 3-1 dhidi ya Uruguay.
  • katika mchuano wa kukata na shoka wa fainali wachezaji magwiji, Pele,Jairzinho,Gerson na Carlos Alberto waliishindia timu yao kwa mabao 4-1 dhidi ya Italia.

  1966:waliokuwa wenyeji wa michuano ni Uingereza ambao walilinyakua kombe kwa mara nyingine.

  • michuano ya Kombe la dunia ilifanyika nchini Uingerezana kikosi cha uingereza kilinyakua ubingwa, kikiwa na tegemeo lake,Bobby Moore,Uingereza ilitoka suluhu ya bila kufungana na Uruguay kabla ya kuichapa Mexico kwa 2-0 na ufaransa 2-0 katika hatua ya makundi.Kisha iliifunga Argentina 1-0 na Portugal 2-1 kisha kukutana na ujerumani magharibi kwenye fainali.
  • Korea kaskazini iliishangaza wapenzi wa soka katika michuano ya kombe la dunia walipoifunga Italia 1-0, hata hivyo furaha yao ilizimwa baada ya kufungwa na Hungary na Portugal.
  • Urusi ilishinda mechi zote tatu katika hatua ya makundi kwa kuiadhibu Korea kaskazini 3-0, Italia 1-0 na Chile 2-1 kabla ya kuichapa Hungary 2-1 katika hatua ya robo fainali.Ujerumani magharibi iliyoichabanga Uruguay 4-0 katika hatua ya robo fainali, iliiondoa urusi katika hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga mabao 2-1
  • Mchezaji wa uingereza Geoff Hurst alifunga mabao matatu katika mchazo wa fainali wakati timu hiyo chini ya kocha wake Alf Ramsey ilipoichapaUjerumani magharibi kwa mabao 4-2 baada ya kipindi cha dakika za nyongeza mbele ya uwanja wa Wembley uliokuwa na mashabiki 98,000

  mwaka 1962, michuano ya kombe la dunia ilihodhiwa na Chile na Brazil ikanyakua ushindi

  • Ikiwa chini ya kocha Walter Winterbottom, England ilitolewa hatua ya robo fainali na Brazil kwa kufungwa mabao 3 - 1. Walianza kwa kufungwa mabao 2 - 1 na Hungary lakini ilijitutumua na kuizaba argentina kwa mabao 3 - 1 na kisha kutoka sare ya bila kufungana na Bulgaria kabla ya kufungwa na Brazil.
  • Czechoslovakia iliingia fainali kwa kuifunga Hispania bao moja kwa bila katika hatua za makundi na kutoka sare ya bila kufungana na Brazil. Uchezaji wao mzuri uliendelea hadi hatua za mtoano baada ya kuifunga Hungary 1 - 0 na kuizaba Yugoslavia 3 - 1.
  • Yugoslavia ilifuta ndoto za Ujerumani Magharibi za kuingia robo fainali baada ya kuifunga 1 - 0, wakati Italia ilishindwa baada ya kufungwa na wenyeji Chile kwa 2 - 0 hivyo kuwagharimu.
  • Brazil waliifunga Chile 4 - 2 katika hatua ya nusu fainali, hivyo kujihakikishia kucheza fainali dhidi ya Czechoslovakia na kuibuka washindi wa mabao 3 - 1.

  1958: Wenyeji Sweden, Mabingwa Brazil.

  • England, Ireland Kaskazini, Scotland na Wales zote zilishiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Sweden mwaka 1958.
  • Ni Ireland Kaskazini pekee na Wales ndizo zilizofika hatua ya robo fainali, ambapo Ireland Kaskazini ilizabwa mabao 4 - 1 na Ufaransa na pia ilipoteza mchezo wake dhidi ya Brazil kwa kufungwa bao 1 - 0. Ireland Kaskazini waliwafunga Czechoslovakia 2 - 1 katika mchezo wa marudiano ili kufuzu robo fainali katika kundi lake, wakati Wales waliichapa Hungary mabao 2 - 1 katika mechi yao ya kwanza.
  • England ambayo ilitoka sare ya mabao 2 - 2 na Soviet Union, 0 - 0 na Brazil na kisha kutoka sare tena ya mabao 2 - 2 na Austria, ilifungwa bao 1 - 0 na Soviet Union katika mechi ya marudiano. Scotland ilishindwa kushinda hata mechi moja, ilitoka sare ya bao 1 - 1 na Yugoslavia na kufungwa mabao 3 - 2 na Paraguay na 2 - 1 dhidi ya Ufaransa.
  • Wenyeji Sweden waliwafunga Soviet Union mabao 2 - 0 na kisha Ujerumani mabao 3 - 1 katika hatua za mtoano, wakati Brazil waliibamiza Ufaransa kwa mabao 5 - 2 katika nusu fainali hivyo kutinga fainali ambapo timu hiyo kutoka Amerika ya Kusini ilitwaa kombe kwa kuifunga Sweden mabao 5 - 2 huku Pele na Vava kila mmoja akipachika wavuni mabao mawili.

  1954:Wenyeji Uswisi, Mabingwa Ujerumani Magharibi.

  • Kilikuwa ni kipigo cha mabao 4 - 1 katika hatua ya robo fainali ambacho England ilipata kutoka kwa Uruguay katika fainali za mwaka 1954, baada ya kutoka sare ya mabao 4 - 4 na Ubelgiji na ushindi wa mabao 2 - 0 dhidi ya Uswisi.
  • Hungary ikiwa na mkongwe Ferenc Puskas, walikuwa ni mwiba katika hatua za makundi baada ya kuizaba Korea Kusini kwa mabao 9 - 0 na kisha Ujerumani Magharibi kwa mabao 8 - 3. Walishinda mchezo mkali dhidi ya Brazil kwa mabao 4 - 2 katika robo fainali kabla ya kuifunga Uruguay kwa mabao 4 - 2 na kupata nafasi ya kucheza fainali.
  • Austria waliifunga Uswisi 7 - 5 katika mchezo uliowashangaza wengi hatua ya nane bora, lakini walipwaya na kufungwa mabao 6 - 1 na Ujerumani Magharibi katika nusu fainali.
  • Ujerumani Magharibi ambao walithibitishwa kuwa wanachama kamili wa FIFA miaka minne mapema, walishinda fainali katika mchezo maridadi kwa kuifunga Hungary mabao 3 -2 licha kuwa nyuma kwa mabao 2 -0 katika dakika nane za mwanzo.

  1950: Wenyeji Brazil, Mabingwa Uruguay.

  • Wakati Scotland ilijitoa kabla hata ya ratiba kupangwa, England ndio walikuwa wawakilishi pekee wa Taifa la Uingereza katika fainali za Kombe la Dunia Brazil mwaka 1950. Hata hivyo, kikosi hicho kilichokuwa chini ya kocha Walter Winterbottom kilifanikiwa kushinda mchezo mmoja tu dhidi ya Chile kwa kuifunga mabao 2 - 0, huku wakitolewa katika mzunguko wa mwanzo baada ya kufungwa bao 1 - 0 na Marekani na pia kupoteza mchezo wake dhidi ya Hispania kwa bao 1 - 0 pia hivyo kuhitimisha ushiriki wao.
  • Timu bora nne za juu kutoka katika kila kundi - Uruguay, Brazil, Sweden na Hispania zilifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali.
  • Brazil walionekana kuwa na neema hasa baada ya kuwazaba Sweden kwa mabao 7 - 1 na kisha Hispania kwa mabao 6 - 1. Uruguay ilitoka sare ya kufungana mabao 2 - 2 na Hispania na walifanikiwa kuifunga Swden 3 - 2 hivyo kutinga fainali.
  • Katika moja ya mechi zilizowashangaza wapenzi wa soka na kubakia katika kumbukumbu za Kombe la Dunia, Uruguay ilikuwa nyuma hadi kipindi cha pili lakini walirejea na kuibuka mabingwa baada ya kuifunga Brazil mabao 2 - 1.

  1938: Mwenyeji ilikuwa Ufaransa na Bingwa ikawa Italy

  • Hakuna timu ya nyumbani iliyocheza mwaka 1938 kombe la dunia Ufaransa mahali ambapo mashindano yalikuwa ni ya mtoano kuanzia mzunguko wa kwanza.
  • Timu ya Dutc East Indies zilikuwa ni miongoni mwa timu zilizokuwa na ushindani ambapo illishindwa kwa magoli 6 - 0 dhidi ya Hungary katika mzunguko wa kwanza. Cuba nayo ilichukua nafasi ambapo iliifunga Romania kabla ya kufungwa 8 - 0 na Sweden katika mzunguko unaofuata.
  • Bingwa mtetezi Italia ilikuwa ni timu ya kufunga nyingine, ilifunga Norway 2 -1 , Ufaransa 3 -1 na Brazil 2 - 1 na kuingia hatua ya fainali.
  • Hungary ambayo ilitandika Sweden 5 - 1 katika hatua ya nusu fainali, iliingia fainali lakini ilifungwa na timu iliyokuwa ikitawala mashindano hayo timu ya Italia.

  1934: Mwenyeji ilikuwa Italia, na Bingwa ikawa Italia

  • Italia ilikuwa mwenyeji wa fainali za pili za Kombe la Dunia ambayo hayakuwa na timu ya nyumbani ambazo zilikuwa zikicheza kwenye mashindano yao ya ndani. Azzurri ikaanza kwa kuifunga Marekani kwa ushindi wa magoli 7 - 1.
  • Labda mshangao ukaja wakati wa ufunguzi pale Hispania ilipoifunga Brazil 3 -1 huku Sweden ikaiondoa Argentina kwa magoli 3 - 2.
  • Czechoslovakia ilifanya kila liwezekanalo kuingia fainali kwa kuifunga Romania 2 - 1 , Uswis 3 - 2 , na Ujerumani 3 - 1.
  • Italia ambayo ilikuwa inahitaji kucheza mechi ya marudio ili kuifunga Hispania kabla ya kuondoa Austria kwa goli 1 - 0, pia iliingia fainali na kunyakua kombe baada ya ushindi wa 2 -1 dhidi ya Czechs katika dakika za nyongeza.

  1930: Mwenyeji ilikuwa Uruguay na Bingwa akawa Uruguay

  • Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia liliandaliwa na Uruguay, na kushirikisha timu 13 hakuna hata timu iliyotoka Uingereza.
  • Argentina ilionekana kutawala mashindano hayo baada ya kuifunga Ufaransa goli 1 - 0, Mexico 6- 3 na Chile 3 -1 katika fainali za nne za Kombe la Dunia.
  • Mwenyeji Uruguay ilikuwa kwenye kiwango kizuri ambapo iliifunga Peru goli 1 - 0 na Romania 4 - 0 kabla ya kuibamiza Yogoslavia 6 -1 katika hatua ya nusu fainali.
  • Mbele ya mashabiki 93,000 Montevideo, Uruguay ilichukua Kombe la Dunia baada ya kumfunga mpinzani wake mkuu Argentina kwa magoli 4 - 2.

  BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

  Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.