Djokovic kucheza fainali

Mchezaji namba moja duniani katika mchezo wa Tennis Novak Djokovic amemshinda mpinzani kutoka Uingereza, Andy Murray na hivyo kujisafishia njia ya kupambana na mtani wake mkuu Rafael Nadl katika pambano la mwisho siku ya jumapili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Novak Djokovic

Hata hivyo ushindi wa Djokovic haukuwa wa mteremko ilimbidi kutumia nguvu yake, maarifa na janja zake zote kumuondoa Murray aliyenuwia leo kumsukuma angalau afike fainali ya mashindano haya ya Australia.

Andy Murray alipigana kufa na kupona baada ya kupoteza seti ya kwanza 6-3 na kushinda ya pili 6-3 na ya tatu 7-6. Baada ya hapo mshindi wa mashindano haya ya Australia mwaka jana aliona kitumbua kimeingia mchanga ndipo akafungua ukurasa tofauti na ule aliyouzowea Murray na kushinda seti ya nne akiandika 2 kwa 2.

Hiyo ikamaanisha mchuano ungalipo. Seti ya tano ilivuta pambano ambapo Djokovic akiongoza 5-2 Muingereza Murray alijitahidi na kubadili mawimbi hadi 5-5 lakini baada ya saa tano na dakika 40 nyota ya raia wa Croatia ikapitia makosa ya mpinzani wake na kujiokotea michezo iliyompa ushindi na fursa ya kufurashana na Rafael Nadal katika fainali siku ya jumapili.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Azarenka baada ya kumshinda Clisters

Fainali ya wanawake ni jumamosi kati ya mshindi wa pambano la Maria Sharapova na Kivitova na baada ya mchuano huo sasa Sharapova atachuana na Viktoria Azarenka kutoka Belarus kumpata bingwa wa wanawake wa Australia open.