Zambia na Libya sare

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Libya na Zambia katika mechi zao za kundi A

Zambia na Libya jana Jumatano zilitoka sare ya 2-2 katika mechi ya iliyochezwa katika uwanja uliokuwa umeloa maji

Hata hivyo mechi hiyo ilikuwa ni wa kuvutia sana na uliojaa misisimko chungunzima.

Mkwaruzano huo ulicheleweshwa kwa karibu saa moja nzima kutokana na uwanja kujaa maji yalisababishwa na mvua kubwa inayonyesha eneo hilo.

Kabla ya kwenda mapumzikoni mshambulizi wa Libya Ahmed Saad Osman aliifungia nchi yake magoli mawili.

Na katika kipindi cha pili Emmanuel Mayuka aliiwafungia vijana wa Chipolopolo bao la kwanza na halafu Christopher Katongo akafanya mambo kuwa 2-2.

Kabla ya hapo mechi hiyo ya kundi A ilionekana kama ingeliahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.