Sudan na Angola sare ya 2-2

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa Angola na wa Sudan wakikabiliana katika mechi yao ya kundi B

Hatimae Sudan walijipatia pointi yake ya kwanza kabisa katika mshindano ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika kwa kutoka sare ya 2-2 na Angola.

Kwa miaka 36 iliyopita, Sudan hawajawahi kupata pointi yeyote.

Walioanza kuona lango la mwenzake ni Angola wakati Manucho alipourukia mpira na kufunga bao kutokana na makosa katika safu ya ulinzi.

Lakini katika dakika ya 30 Mohammed Bashir aliifungua Sudan bao lake la kwanza.

Baadae Manucho alipofunga bao kupita mkwaju wa penalti, Bashir tena alijibu kwa kupachika bao na kufanya mabao kuwa 2-2.

Sare hii imeufurahisa Sudan kwani tangu mwaka wa 1970 waliposhinda kombe hilo , kiwango chake cha mpira umekuwa ukishuka.

Baada ya kutoshiriki katika mashindano hayo katika kipindi cha miaka 32, mwaka wa 2008 walirudi tena wakati yalipoandaliwa nchini Ghana.

Katika mashindano hayo ya Ghana ya mwaka 2008 , Sudan walirudi nyumbani baada ya kushindwa mechi zote na bila kufunga bao lolote.

Hivyo basi sare hii na timu ya Angola ni jambo la kujivunia.