Guinea na Botswana nje!

Ghana ilijitengea nafasi yake katika robo fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kutoka sare 1-1 na Guinea katika uwanja wa Franceville.

Haki miliki ya picha
Image caption Timu ya Ghana ilifanikiwa kuongoza kundi D baada ya kwenda sare na Guinea

Emmanuel Agyeman Badu aliweza kupata bao la kwanza katika mechi hiyo.

Abdoul Razzagui Camara hata hivyo alisawazisha bao hilo mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Guinea walijitahidi kupata bao la ushindi, lakini hawakufanikiwa.

Ushindi wa Mali wa magoli 2-1 dhidi ya Botswana ulimaanisha Guinea wanaondoka pasipo kucheza robo fainali.

Mechi kati ya Mali na Botswana ilichezewa mjini Libreville.

Botswana ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia Mogakolodi Ngele, bao la ufundi mkubwa, na ambalo kipa Oumar Sissoka hakujui ni nini kimepita hadi wavuni.

Garra Dembele aliweza kuisawazishia Mali, kabla kiungo cha kati Seydou Keita kumaliza kazi kwa bao la ushindi.

Ushindi huo ulimaanisha kwamba Mali ilimaliza katika nafasi ya pili katika kundi D, nyuma ya Ghana.

Timu zitapumzika siku mbili, kabla mapambano mawili ya kwanza ya robo fainali kuchezwa siku ya Jumamosi.