Bendtner ahofia angekuwa kipofu

Mshambuliaji wa Sunderland Nicklas Bendtner, amesema alikuwa na wasiwasi huenda amepoteza uwezo wa kuona alipoumia jicho katika mechi dhdi ya Swansea City mwezi wa Januari.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Nicklas Bendtner alihofia upofu

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark alipelekwa hospitali baada ya mfupa juu ya jicho lake kuvunjika alipokumbana na mlinzi wa Swansea Angel Rangel.

"Nafurahi kwamba sikupofuka," Bendtner aliiambia BBC.

"Sikuweza kulitumia jicho langu kwa saa nne au tano na pia nililazimika kulazwa hospitalini usiku kucha."

Bendtner, anayechezea Sunderaland kwa mkopo akiwa mchezaji wa Arsenal hadi mwishoni mwa msimu, alifunga bao la kuongoza wakati timu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle United siku ya Jumapili.

Mbali ya kurejea katika mechi dhidi ya West Bromwich Albion wiki moja kabla, mshambuliaji huyo hakucheza kandanda kwa muda wa mwezi mmoja alipokuwa akijiuguza na katika mechi mbili zilizopita alikuwa amevaa kifaa maalum cha kukinga uso.

Alisema "Sijali kugongwa au kuvunjika pua ama taya ambayo yatapona tu, lakini macho yako ni muhimu zaidi".

"Mara tu nilipogongwa, sikuweza kuona kitu chochote na mawazo yaliyonijia awali nimepofuka', kwa hiyo nilifarijika kupita kiasi, kwa kutumia mikono yangu, niliweza kufunua jicho na kuona vitu vingi vyekundu.

"Natumai kuna malaika anayelinda.