Podolski kujiunga na Gunners

Lukas Podolski
Image caption Lukas Podolski

Klabu ya Arsenal imeafikiana na mshambuliaji wa Ujerumani Lukas Podolski kutoka klabu ya Cologne, BBC Michezo imefahamu.

Kwa mujibu wa taarifa Arsenal italipa pauni za Uingereza £10.9m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa mkataba wa miaka minne akilipwa pauni £100,000 kila wiki.

Hata hivyo itabidi Podolski amalize utaratibu wa afya yake na kukubaliana juu ya maslahi yake kabla kuhamia London majira ya joto mwaka huu.

Image caption Lukas Podolski

Beki wa Arsenal Per Mertesacker amesema kua: "amekua akiwasiliana nami mara kwa mara na nilimfahamisha kuhusu vifaa na kwamba ni mahali pazuri kufanyia kazi na klabu ya Arsenal ni nzuri sana.

Wachezaji hao wamecheza pamoja katika Timu ya Taifa ya Ujerumani tangu mwaka 2004 na wanatazamia kushirikiana katika klabu moja.

Meneja wa klabu ya Cologne Stale Solbakken alikiri mwezi uliopita kua huenda akampoteza mshambuliaji wake huyo Podolski kwa Arsenal na kuongezea kua shughuli za kumsajili zimefikia hatua pevu.