Man City yanyolewa Ureno.

Itailazimu timu ya Manchester City kujikakamua na kuifunga Sporting Lisbin ya Ureno wiki mbili zijazo baada ya kuchapwa 1-0 ugenini.

Haki miliki ya picha GOOGLE
Image caption Sporting Lisbon washerehekea kwa kuichuna Man City

Hii ilikuwa ni katika mechi za timu 16 bora katika kinyang'anyiro cha kombe la Euro.

Man City walitoka uwanjani wakiwa wanyonge baada ya kuchezewa na vijana wa Ureno ambao walikuwa wakionana vizuri.

Bao la kwanza na la pekee la Sporting lilifungwa na mara tu baada ya kipindi cha lala salama kuanza.

Wadadisi wa soka wanadai kuwa licha yakufungwa huko ,bado Man City inanafasi nzuri ya kuifunga Sporting Lisbon na hatimae kusonga mbele katika michuano hiyo ya kombe la Europa