Nova2010 FC yachapwa 58-0

Wakuu na wachezaji wa timu moja inayocheza soka ya mitaa au bustani, wanajitahidi kutathmini kilichotokea na kusababisha kinachoaminika kua kipigo kikubwa kuwahi kutokea katika mpira wa miguu katika historia ya Uingereza.

Klabu ijulikanayo kama Nova 2010 FC iliadhibiwa kwa kuchapwa 58-0 dhidi ya watani wa mji ule ule Wheel Power FC katika Ligi ya Torbay Sunday League huko Devon.

Mambo yalianza mapema kwa Nova na kuendelea kuwa hivyo hata kufikia mapumziko ikiwa Nova imeisha bugia 20-0 kabla ya kipindi cha pili kushuhudia mengine 38.

Inaaminika kua ushindi wa Wheel power ndiyo mkubwa kuwahi kuandikwa, baada ya ushindi wa awali wa Timu ijulikanayo kama Illogan wa mabao 55-0 dhidi ya Madron FC mwezi novemba mwaka 2010

Mchezaji mmoja ka jina Lewis Parker, akiwa na umri wa miaka 60-anayeichezea Nova 2010, alisema kua wachezaji wengi hawakujitokeza kwa hio tulitarajia matokeo mabovu ingawa si kiasi hiki.

Nova ilipofika uwanjani bila wachezaji wake wa kawaida ndipo ikakusanya watu wengine watano na kutumia jumla ya wachezaji tisa pekee dhidi ya Timu inayoongoza Ligi hio ya Torbay.

Ndugu wawili Robbie mwenye umri wa miaka 27 na Bowker mwenye umri wa miaka 21 walifunga jumla ya mabao 28 ambapo Robbie alifunga 18 na Bowker kufunga 10.