Alonzo ashinda mbio Malaysia

Fernando Alonso Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Fernando Alonso

Fernando Alonso wa Timu ya magari ya Ferrari ameshinda mashindano ya mbio za magari ya Langalanga yaliyofujwa na mvua kali ya Malaysia.

Dereva huyo alimaliza kwa kasi akijitahidi kumuacha Sergio Perez wa magari ya Sauber aliyetishia kumuondoa kileleni lakini hadi mwisho Alonso akashikilia nafasi ya

kwanza.

Gari la Ferrari linasumbuliwa na uwanja ulio kauka na baada ya mashindano kusimamishwa kutokana na mvua kali, yalipo anza akatumia fursa hio kumpiku Hamilton ambaye hadi kusimama kwa mbio hizo alikua akiongoza.

Perez aliyetishia kushinda mbio hizi kwa jinsi alivyoendesha gari lake alikosea njia na kupoteza mda na kukubali nafasi ya pili.

Lewis Hamilton wa magari ya McLaren alimaliza wa tatu mbele ya Mark Webber wa Red Bull na Dereva wa Lotus Kimi Raikkonen. Kabla ya mbio hizi magari ya Ferrari yalidhaniwa kua na matatizo mengi kufuatia matokeo mabovu katika mbio za kwanza za msimu huko Australia wiki moja kabla, lakini uwezo uliodhihirishwa katika mazingira ya mvua yalimpa bingwa wa mara mbili Alonzo fursa ya ushindi wa kujivunia.

Lewis Hamilton aliyeongoza mashindano haya alimaliza wa tatu na Alonzo kusema baada ya mashindano hayo kua, 'ni miujiza na kazi nzuri ya timu nzima ya Ferrari.Hatukudhani kama tunaweza kushinda baada ya matokeo ya Australia.

Image caption Fernando Alonso

Hamilton alisema kua timu yao ya McLaren ingefurahia kuzoa pointi zaidi kwenye mashindano haya mfululizo -lakini, siwezi kulalamika, nashukuru nimeweza kumaliza na kupanda jukwaa kwa mara ya pili mfululizo.

Dereva mgeni wa Timu ya magari ya Williams, Bruno Senna alimaliza wa sita, Paul di Resta wa saba Jules Vergne wa Toro Rosso wa nane na Nico Hulkenberg akimaliza wa tisa.

Bingwa wa mara nyingi mkongwe wa mashindano haya Michael Schumacher alijinyakulia pointi ya mwisho kwa kumaliza wa kumi.

Bingwa mtetezi Sebastien Vettel wa Red Bull alikua nyuma ya Hamilton katika nafasi ya nne kwa kipindi kirefu cha mashindano lakini tairi lake lilipasuka baada ya gari lake kubusu gari la Narain Karthikeyan na kuridhika na nafasi ya 11 bila kuzoa pointi hata moja.

Jenson Button wa magari ya Maclarena aliyeshinda mbio za Australia wiki moja kabla ya Malaysia alimaliza wa 14 baada ya gari lake hapo mapema katika mbio kukwaruzana na gari la Karthikeyan wa Force India.

Fernando Alonso wa Timu ya magari ya Ferrari ameshinda mashindano ya mbio za magari ya Langalanga yaliyofujwa na mvua kali ya Malaysia.

Dereva huyo alimaliza kwa kasi akijitahidi kumuacha Sergio Perez wa magari ya Sauber aliyetishia kumuondoa kileleni lakini hadi mwisho Alonso akashiki

lia nafasi ya kwanza.